MWANAMKE anapopata ujauzito kwa kawaida
huwa anaanza kuona dalili ambazo si za
kawaida. Na ni wakati huo ambao ni muafaka
kwake kuanza kuuchunguza mwili wake
.


Maumivu kwenye matiti:
Hii ni dalili ya kawaida ya ujauzito ambapo
nguvu za homoni mwilini huongezeka wakati
yai linavyopata “rutuba”, jambo ambalo
huongeza wingi wa damu na kuyafanya
matiti ya mwanamke kuvimba na kuwa
makubwa isivyo kawaida.

Maumivu mwilini:
Utaanza kusikia maumivu kama vile unataka
kuingia katika siku zako. Kwa kawaida hali hii
hutokea wakati yai likiwa linasafiri kwenda
katika chumba cha mimba. Hivyo, hali hiyo
husababisha sehemu hiyo itanuke taratibu na
kusababisha maumivu hayo.

Kutokwa damu bila kutegemea:
"Wanawake wengi hufikiria kutokwa na
damu kidogo ni dalili ya kuwa katika siku zao.
Lakini, katika hali halisi, kutokwa damu
kusikotegemewa, huwakumba asilimia 25 ya
wanawake wakati wa kurutubika kwa yai,”
iwapo utaona hedhi yako inakuwa
fupi au inafanyika katika hali ambayo si ya
kawaida, unashauriwa kwenda kufanya
kipimo cha ujauzito.

Kuchoka:
Unapojisikia kuchoka na kukosa raha, au
kutaka hata kulala wakati ukiwa kazini, lazima
ufahamu kwamba mwili wako unajirekebisha
kuingia katika kipindi kipya cha mabadiliko.
“Tambua kwamba katika kipindi cha mwanzo
cha ujauzito ni muda ambao mtoto tumboni
huanza kutumia sehemu ya nguvu zako na
hivyo kukuletea uchovu na usingizi”

 
 Chuchu kuwa nyeusi:
Chuchu huanza kubadilika rangi yake
kutokana na chembechembe za uhai (seli)
kuanza kufanya kazi kwa nguvu zaidi. Hata
hivyo, 
 “Wanawake wenye
ngozi nyeusi hawawezi kuiona dalili hii
mapema hadi muda wa kama wiki kumi
zipite.”

Kichefuchefu:
Hali hii huwapata asilimia 85 ya wanawake
wanapopatwa na ujauzito, ambapo nyakati za
asubuhi ndipo hasa hujionyesha.

Mwili kuvimba:
Kuna wakati kupungua kwa nguvu za
uyeyushaji chakula kunaweza kukusababishia
kuona tumbo limevimba na nguo zikawa
zinakubana kutokana na chakula kujaa katika
utumbo. Lakini hali hiyo ikiendelea na ukaona
siku zako haziji, basi ni vyema ukatambua
kwamba tayari una ujauzito na
kinachokupasa ni kwenda kuhakikisha.

Kwenda haja ndogo mara kwa mara:
Kwenda haja ndogo kila mara ni dalili
kwamba kibofu chako kimeanza kufanya kazi
ya ziada, ambapo huwa kinafanya kazi ya
kuondoa maji kwa uthabiti zaidi wakati wa
ujauzito. Hali hii pia hujitokeza mwishoni
mwa ujauzito, ambapo kibofu kitakapokuwa
kinarudia hali yake ya kawaida baada ya
kufanya kazi kwa muda mrefu.

Tamaa ya vitu mbalimbali:
Kutokana na mwili kuwa na “mzigo” wa
ujauzito na hivyo kuchoka, hali hiyo humfanya
mwanamke kutamani vitu mbalimbali ili
kukidhi mabadiliko yaliyojitokeza katika mwili
wake. Hii ni pamoja na kutaka vyakula fulani
au kufanya mambo ambayo hapo nyuma
alikuwa hayapendi.

Kuumwa kichwa:
Kuongezeka kwa damu kunaweza
kusababisha kichwa kuuma japokuwa si
sana, hususani katika wiki za mwanzo za
ujauzito. Hata hivyo, hali hii hukoma mwili
unapojirekebish a na mzunguko wa homoni
unaotokana na ujauzito.

Kufunga choo:
Homoni ambazo husababisha mwili kuvimba
pia husababisha kufunga choo kutokana na
mfumo wa kuyeyusha chakula kutofanya kazi
vyema. Hata hivyo hali hii inaweza kujitokeza
zaidi wakati ujauzito unapoendelea kukua.

Kuwa na hasira
"Kutokana na kuongezeka kwa homoni za
utendaji kazi mwilini, hali hiyo
itakusababishia uchovu, na kukufanya kuwa
na hasira,” 

Kuongezeka kwa joto mwilini:
Kipimo cha joto la mdomo ni muhimu katika
kutambua hali ya ujauzito. Kwa kawaida joto
huongezeka kwa nyuzi moja au zaidi wakati
yai likiwa linatunga mimba. Hali hiyo
ikiendelea kwa zaidi ya wiki mbili, itakuwa
inaonyesha dhahiri kwamba kuna “mtoto
anakuja”.

Post a Comment

POPULAR POST

 
Top