UKWELI KUHUSU MAJINI
Kuhusu majini kuna majini wema na wabaya
(a) Majini wema.
1.Majini wema awamuingii mtu na kumlazimisha mambo kwani hiyo ni dhuluma.
2.Humpatia mtu mambo mazuri yale anayo hitaji mtu mwenyewe kwa mfano:- utajiri na Nk.
(b) Majini wabaya ni wale waliomuhasi mungu hao hujiita mashetani.
1.humuingia mtu au hukaa maeneo anayoishi
2.Hutumika na watu wabaya kuwapelekea watu wengine,kuaribu maisha ya mtu au asifanikiwe na jambo fulani.
DALILI ZA MTU MWENYE SHETANI WA KIJINI
Mtu anaweza kuwa na shetani wa kijini na asijitokeze na ikiwa anasumbuliwa na maumivu tu,mtu huyo na akamaliza matibabu ya hospitali bila ya mafanikio.
ZIFATAZO NI BAADHIYA DALILI ZA MTU MWENYE SHETANI WA KIJINI
1.Kuumwa kichwa upande mmoja,masikio,meno,mgongo,kiuno na kubwana kifua.
2.Kuumwa tumbo chini ya kitovu kwa wakinama mama.
3.Moyo kwenda mbio na kushtuka bila sababu.
4.Kushika moto mwili hasa miguu pamoja na ganzi na maumivu makali.
5.Kizunguzungu.
6.Kuumwa tumbo sana akina mama wakati wa hedhi pamoja na kutoa damu nyingi au damu chache sana.
7.Akina mama kupata maumivu sana ya tendo la ndoa na kukosa hamu ya tendo hilo na kulichukia.
8.Kutembea vitu mwilini.
9.Kutingishika bila sababu na kutetemeka pamoja na kulia bila sababu ikiwemo na hasira sana.
10.Kuhisi uzito wa mwili kama umebeba mzigo mzito.
11.Chuki ndani ya ndoa kutamani kuacha au kuachwa bila sababu.
12.Maneno machafu kwa mwenza na punde tu majuto.
13.Kufunga hedhi bila ujauzito na kutopata ujauzito bila sababu za msingi.
14.Kuota ujauzito unazaa unanyonyesha unabeba watoto.
15.Kujaa tumbo mfano ujauzito na kucheza kitu tumboni bila ujauzito.
16.Kuharibika mbimba baada ya kuota tendo la ndoa na mtu atishae.
17.Kuyeyuka mimba na kuharibika bila sababu za msingi.
18.Ndoto za tendo la ndoa mara kwa mara.
19.Kuwa na hamu ya tendo la ndoa uwapo peke yako lakini ukutanapo na mwenza wako hamu utoweka na kwa mume hupotelewa nguvu.
20.Kuvurugikiwa mipango ya kuoa au kuolewa mara kwa mara.
21.Kujihisi unaingiliwa siyo ndotoni.
22.Kutopenda ibada na kupenda maasi.
23.Kuhisi kusimamiwa na mtu mbele yako,nyuma,pembeni na hata ulalapo kuwa na hofu sana juu ya hilo.
24.Hasira, uvivu pamoja na hofu bila sababu.
25.Kukosa usingizi au usingizi mzito mpaka una shindwa kuamka asubuhi na mapema.
26.Usingizi wakati wa kusoma au kusikiliza manbo ya maana lakini mambo ya kipuuzi au kusoma magazeti ya udaku havikuletei usingizi.
27.Tamaa kupita kiasi na kujihisi mtu wa samani sana kinyume na ilivyo.
28.Mwanamke kupenda kujipambo awapo nje ya nyumba yake na hajipambi mbele ya mumewe.
29.Kupenda vitu vya kipuuzi kama porojo,muziki,magazeti ya udaku,vipindi vya TV au
RADIO visivyo na maana na kuacha vile vyenye maana.
30.Kuota ndoto za vitisho kama wanyama wakali au unafanyiwa uadui au umezingirwa na maji,kifo,jeneza,unatumbukia shimoni na unapaa hewani.
31.Kuota ibada zisizo na muelekeo.
32.Kulia,kusema,kucheka,na kupiga kelele usingizini (JINAMIZI)
33.Kuchanganyikiwa ndani ya sala pamoja na kuyumba na kusinzia.
34.Kuota mtu amekufa au unaelezwa jambo ndotoni na ikawa yote ni kweli hali huna uchamungu wa ivyo.
35.Kuota watu watishao.
36.Kuota sana nyumba za ibada hali ya kuwa wewe si mtu wa ibada.
37.Kuota unafanya mashauri na watu walio kufa.
38.Kuota unafanyiwa shughuli zote za mazishi au unafanyia mtu mwengine (MZIMU)
39.Kuota unaingiliwa kinyume na maumbile.
40.Kushtuka mara kwa mara usingizini.
41.Kuibiwa pesa hata zifungiwe ndani ya droo.
Dalili hizi zinaashiria mtu kuwa na shetani siyo lazima awe nazo zote hata awe nazo baadhi tu.
1. Kutojiamini au kujiamini kupita kiasi
2.Mtu kuwa na wasiwasi
3.Kuota ndoto zikatokea kama ulivyoota
4.Kusema peke yako
5.Kusisimkwa mwili ua kutambaliwa na vitu kama sisimizi mwilini
6.Kusikia baridi sana au joto sana
7.Kupenda sana watoto
8.Ndoto za kua baharini
9.Kupitiwa na upepo ghafla au pulizo
10.Kutopenda tendo la ndoa
11.Kuota una mali nyingi sana
12.Kuwa na hasira sana
13.Kuota una mimba au unalea mtoto
14.Macho kua kiza ghafla na kurudi hali yake
15.Midomo kucheza cheza
16.Kusahau sahau mara kwa mara
Hizi ni baadhi tu ya dalili kuu za mtu kuwa na majini mwilini mwake ima wazuri au wabaya zipo dalili nyingi sana.

Post a Comment

POPULAR POST

 
Top