UKWELI KUHUSU MAJINI
Kuhusu majini kuna majini wema na
wabaya
(a) Majini wema.
1.Majini wema awamuingii mtu na
kumlazimisha mambo kwani hiyo ni dhuluma.
2.Humpatia mtu mambo mazuri yale
anayo hitaji mtu mwenyewe kwa mfano:- utajiri na Nk.
(b) Majini wabaya ni wale waliomuhasi
mungu hao hujiita mashetani.
1.humuingia mtu au hukaa maeneo
anayoishi
2.Hutumika na watu wabaya kuwapelekea
watu wengine,kuaribu maisha ya mtu au asifanikiwe na jambo fulani.
DALILI ZA MTU MWENYE SHETANI WA
KIJINI
Mtu anaweza kuwa na shetani wa kijini
na asijitokeze na ikiwa anasumbuliwa na maumivu tu,mtu huyo na akamaliza
matibabu ya hospitali bila ya mafanikio.
ZIFATAZO NI BAADHIYA DALILI ZA MTU MWENYE SHETANI WA KIJINI
1.Kuumwa kichwa upande
mmoja,masikio,meno,mgongo,kiuno na kubwana kifua.
2.Kuumwa tumbo chini ya kitovu kwa
wakinama mama.
3.Moyo kwenda mbio na kushtuka bila
sababu.
4.Kushika moto mwili hasa miguu
pamoja na ganzi na maumivu makali.
5.Kizunguzungu.
6.Kuumwa tumbo sana akina mama wakati
wa hedhi pamoja na kutoa damu nyingi au damu chache sana.
7.Akina mama kupata maumivu sana ya
tendo la ndoa na kukosa hamu ya tendo hilo na kulichukia.
8.Kutembea vitu mwilini.
9.Kutingishika bila sababu na
kutetemeka pamoja na kulia bila sababu ikiwemo na hasira sana.
10.Kuhisi uzito wa mwili kama umebeba
mzigo mzito.
11.Chuki ndani ya ndoa kutamani
kuacha au kuachwa bila sababu.
12.Maneno machafu kwa mwenza na punde
tu majuto.
13.Kufunga hedhi bila ujauzito na
kutopata ujauzito bila sababu za msingi.
14.Kuota ujauzito unazaa unanyonyesha
unabeba watoto.
15.Kujaa tumbo mfano ujauzito na
kucheza kitu tumboni bila ujauzito.
16.Kuharibika mbimba baada ya kuota
tendo la ndoa na mtu atishae.
17.Kuyeyuka mimba na kuharibika bila
sababu za msingi.
18.Ndoto za tendo la ndoa mara kwa
mara.
19.Kuwa na hamu ya tendo la ndoa
uwapo peke yako lakini ukutanapo na mwenza wako hamu utoweka na kwa mume
hupotelewa nguvu.
20.Kuvurugikiwa mipango ya kuoa au
kuolewa mara kwa mara.
21.Kujihisi unaingiliwa siyo ndotoni.
22.Kutopenda ibada na kupenda maasi.
23.Kuhisi kusimamiwa na mtu mbele
yako,nyuma,pembeni na hata ulalapo kuwa na hofu sana juu ya hilo.
24.Hasira, uvivu pamoja na hofu bila
sababu.
25.Kukosa usingizi au usingizi mzito
mpaka una shindwa kuamka asubuhi na mapema.
26.Usingizi wakati wa kusoma au
kusikiliza manbo ya maana lakini mambo ya kipuuzi au kusoma magazeti ya udaku
havikuletei usingizi.
27.Tamaa kupita kiasi na kujihisi mtu
wa samani sana kinyume na ilivyo.
28.Mwanamke kupenda kujipambo awapo
nje ya nyumba yake na hajipambi mbele ya mumewe.
29.Kupenda vitu vya kipuuzi kama
porojo,muziki,magazeti ya udaku,vipindi vya TV au
RADIO visivyo na maana na kuacha vile
vyenye maana.
30.Kuota ndoto za vitisho kama
wanyama wakali au unafanyiwa uadui au umezingirwa na maji,kifo,jeneza,unatumbukia
shimoni na unapaa hewani.
31.Kuota ibada zisizo na muelekeo.
32.Kulia,kusema,kucheka,na kupiga
kelele usingizini (JINAMIZI)
33.Kuchanganyikiwa ndani ya sala
pamoja na kuyumba na kusinzia.
34.Kuota mtu amekufa au unaelezwa
jambo ndotoni na ikawa yote ni kweli hali huna uchamungu wa ivyo.
35.Kuota watu watishao.
36.Kuota sana nyumba za ibada hali ya
kuwa wewe si mtu wa ibada.
37.Kuota unafanya mashauri na watu
walio kufa.
38.Kuota unafanyiwa shughuli zote za
mazishi au unafanyia mtu mwengine (MZIMU)
39.Kuota unaingiliwa kinyume na
maumbile.
40.Kushtuka mara kwa mara usingizini.
41.Kuibiwa pesa hata zifungiwe ndani
ya droo.
Dalili hizi zinaashiria
mtu kuwa na shetani siyo lazima awe nazo zote hata awe nazo baadhi tu.
Post a Comment