Mbwa anayenyonyesha watoto wa Nguruwe Iringa .
Mchungaji Daniel Kisonga akimwonyesha mbwa anayenyonyesha watoto wa Nguruwe
Mbwa huyo akinyonyesha watoto wa Nguruwe huku mtoto wake (kulia) akishindwa kunyonya
Huyu ndie Mbwa anayenyonyesha watoto wa Nguruwe Iringa
Japo
upande wa wadau mbali mbali wamehoji nguruwe hao iwapo wataendelea
kunyonya maziwa na mbwa wataliwa na binadamu ama lah ! kutokana na
nyama ya mbwa kwa kawaida kutoliwa na binadamu sasa iweje kwa
nguruwe hao kunyonya maziwa ya mbwa
Mchungaji Daniel Kisonga akimwonyesha mbwa anayenyonyesha watoto wa Nguruwe
Mbwa huyo akinyonyesha watoto wa Nguruwe huku mtoto wake (kulia) akishindwa kunyonya
Huyu ndie Mbwa anayenyonyesha watoto wa Nguruwe Iringa
Katika
hali isiyo ya kawaida kuzoeleka ni baada ya wakazi wa Ilala
katika Manispaa ya Iringa leo kushuhudia maajabu ya dunia baada ya
kushuhudia tukio la aina yake kwa mbwa kuwachukua watoto wa nguruwe
na kuwalea kwa kuwanyonyesha maziwa yake.
Tukio
hilo limetrokea machi 15 mwaka huu majira ya asubuhi baada ya
nguruwe wa mmoja kati ya watumishi wa mungu (mchungaji ) Daniel
Kisonga kushuhudia mbwa huyo ambae alikuwa amezaa watoto watatu na
kufariki wawili na kubakia na mtoto mmoja na hivyo kulazimika
kuingia katika banda la nguruwe na kubeba watoto wanne wa nguruwe na
kuamua kuwalea na kuwapa huduma zote ikiwemo ya kuwanyonyesha kwa
upendo watoto hao wa Nguruwe bila kuwadhuru.
Akizunguza
na mwandishi wa habari hizi leo mchangaji Kisonga amesema kuwa ni
vigumu kuamini kuna mbwa akinyonyesha watoto wa nguruwe wakati kwa
kawaida mbwa amekuwa ni mnyama hatari kwa nguruwe hao hasa pale
wanapozaliwa .
Amesema
kuwa mbwawa wamekuwa wakiingia katika mazizi ya nguruwe na kuwala
nguruwe hao baada ya kuzaliwa ila imekuwa tofauti kwa mbwa baada ya
kuamua kulea watoto wa nguruwe .
Hata
hivyo amesema yawezekana ni maajabu ya dunia ila pia yawezekana ni
dalili za siku ya mwisho kama ambavyo zimepatwa kutabiliwa katika
maandiko matakatifu kuwa siku za mwisho yatajitokeza mambo mengi ya
ajabu ambayo binadamu ni vigumu kuamini mambo hayo.
Post a Comment