Baada ya Mahakama kutupilia mbali shauri lao hii ikiwa ni mara ya tatu kwa juhudi zao kugonga mwamba, Babu Seya akiwa anapelekwa kwenye gari kurudishwa gerezani na mwanae kuendelea na kifungo cha maisha jela, alitoa kauli ambayo hakuitolea  ufafanuzi zaidi kwa kusema 'kwa binadamu ni makosa lakini kwa Mungu hakuna makosa’ nae Papii Kocha alisema ‘sasa tunamuachia tu Rais ndie anaweza kutoa uamuzi wa mwisho’  
Wafungwa hao, kupitia kwa wakili Mabere Marando walikuwa wakiiomba Mahakama ya rufaa ifanye marejesho ya hukumu iliyotolewa Februari 11, 2010 Iliyothibitisha adhabu hiyo waliyohukumiwa lakini jana, Mahakama ya Rufani katika uamuzi wake uliotolewa na jopo la majaji, uliongeza machungu kwa wafungwa hao pamoja na ndugu , jamaa, na marafiki baada ya majaji hao kulitupilia mbali ombi lao na kuwataka kuendelea na hukumu hiyo.

Post a Comment

POPULAR POST

 
Top