Kipanda
uso (Migraine) ni ugonjwa au maumivu makali ya kichwa anayokuwa nayo
mtu baada ya mshipa wa damu (Enlargement of Artery ) kutanuka katika
kichwa chake. Baada ya kutanuka kwa mishipa hii ya damu, pia kuna
kemikali ndani ya mwili zinazozalishwa na kuizunguka mishipa hii na
kupelekea mtu apate maumivu makali ya kichwa na kutanuka zaidi kwa
mishipa.
Maumivu
makali ya kichwa hupelekea mfumo wa utendaji kazi wa mwili pia
ubadilike, mtu atapatwa na kichefuchefu, kutapika, kuharisha, katika
utumbo chakula hakitanyonywa vizuri kiingie mwilini, mtu atashindwa
kuona vizuri maeneo yenye mwanga na kutopenda kukaa mazingira yenye
sauti au kelele.
Vipo
vitu mbalimbali vinavyoweza kuchangia mtu apate tatizo la kipanda uso,
vitu hivi haimaanishi kuwa ni lazima vikusababishe upate na hata kama
haupo katika mazingira ya vitu hivi haimaanishi kuwa huwezi kupata
tatizo la kipanda uso, miongoni mwa vitu hivyo ni kama vile: sauti kali
au kelele, harufu kali, aleji, mwanga mkali, kuvuta sigara, matatizo ya
kukosa usingizi, kukaa bila kula kwa muda mrefu, pombe, kubadilika
badilika kwa siku za mwanamke (menstrual cycle fluctuations).
Inawezekana
ukawa na tatizo hili la kipanda uso, miongoni mwa vitu vinavyowasaidia
watu wenye kipanda uso ni kutumia dawa mbalimbali ukijumuisha dawa za
maumivu zenye mchanganyiko na caffeine, pia utumiaji wa chai au kahawa umesaidia baadhi ya watu kuwapa nafuu ya maumivu makali ya kichwa.
Tunaweza
kupunguza hatari (risk) ya kupata kipanda uso kwa kubadilisha staili ya
maisha yetu ya kila siku, kuepuka vitu vyenye harufu kali, kuepuka
utumiaji wa tumbaku (sigara), kupata muda wa kutosha kuupumzisha mwili
(kulala), kufanya mazoezi, kutokaa bila kula kwa muda mrefu, kunywa maji
ya kutosha.
Je, unalo tatizo la kipanda uso (Migraine), dalili zako ni zipi na ni vitu gani ukitumia unapata nafuu ?.
Post a Comment