Binti wa miaka nane aitwaye Alani Santos kutoka mji wa San Gonzalo nchini Brazil ameendelea kukusanya mamia ya watu kutoka sehemu mbalimbali nchini kwake ambao hufika kanisani anakoabudu ambako baba
yake ni mchungaji ili waombewe na binti huyo anayeaminika kuwa na nguvu za ajabu za kukemea mapepo na kuponya magonjwa akitumia jina la Yesu.


Katika mji anaotokea binti huyo unaweza kufananisha na Mbeya kwa hapa Tanzania kutokana na kuwa na utitiri wa makanisa licha ya kwamba nchi hiyo kwa sasa inakabiriwa na tishio la watu kutopenda masuala ya kiimani. Brazil taifa ambalo linasifika kuwa la Kikristo wa kanisa la Katoliki, limekuwa na vipaji mbalimbali kupitia watoto akiwemo kijana.

Post a Comment

POPULAR POST

 
Top