Mfano wa banda la ghorofa lenye nafasi ya kuku 100 (Picha na Mamachi Agribusiness)


Huu ni ufugaji wenye tija na katika eneo dogo.
*Eneo linalohitajika ni mita mbili (2), Kwa maana ya Urefu wa mita mbili(2) na Upana wa mita moja(1).


*Kinakachofanyika katika hilo eneo ni ujenzi wa ghorofa/shelves tano(5) kwenda juu kwa ajili ya kufugia kuku.


*Urefu unaoshauriwa wa kila shelf/chumba kimoja ni futi moja na nusu hadi mbili.
*Katika kilachumba/shelf unashauriwa kuweka kuku ishirini, kwa maana ya kuku 10 katika eneo la mita 1.


*Ukichukua idadi ya kuku katika kila chumba (20) mara idadi ya vyumba 5, watapatikana kuku mia(100) katika eneo la mita 2.


*Kumbuka kuwa unaweza kufanya mabadiliko mengine kulingana na eneo utakaloweka ghorofa la kuku.


Vifaranga vya kuku huwekewa chakula katika vyombo vidogo


Usiogope, kuna nafasi ya kutosha kuruhusu ukuaji wa kuku

Post a Comment

POPULAR POST

 
Top