Jinzi chembechembe umbile za kijusu cha binadamu zinavyo ongezeka na kufikia trillioni 100 kwa mtu mzima,labda ni jambo moja la kustaajabisha zaidi kati ya maumbile duniani kote.
Wanautafiti wanafahamu kwamba nyingi ya Kazi za kawaida zinatotekelezwa na mwili wa binadamu zinamarishwa wakati wa ujauzito- mara mingi, muda mrefu kabla ya kuzaliwa kwa mtoto.
Ukuaji wa kijusu kabla ya kuzaliwa inaendelea kufahamika kuwa ni wakati ya utaharishaji ambapo kijusu umbile upata viungo vingi na kuanza kujizoesha mbinu tekelezi zitakazohitaji maishani, mara baada ya kuzaliwa.


Ujauzito kwa binadamu , kwa kawaida Udumu takribani wiki 38 kuanzia siku ya kwanza Wa kutunga mimba hadi kuzaliwa.
Katika wiki 8 za kwanza ukuaji wa kijusu cha binadamu huitwa embryoni(embryo) na humaanisha "kukua ndani". wakati huu, huitwao wakati wa kiembryoni, huhusishwa na kuambwa Kwa mifumo muhimu ya viungo vya mwili.
Kuanzia wiki ya 8 hadi mwisho wa mimba " binadamu umbile uitwa kijusu" kinacho maanisha "mwana ambaye hajazaliwa" Katika wakati huu, huitwao wakati wa ujusu, mwili hukua zaidi na Sehemu zake kuanza kufanya kazi.
umri wa kiembroyoni na ujusu katika mpangilio huu humaanisha wakati tangu utungaji wa mimba.
Awamu ya kwanza
  • Moyo huanza kupiga
  • Kichwa, mikono, vidole vya miguu viungo vingine mishipa ya fahamu zinatengenezwa.
  • Nywele zinaanza kumea
  • Awamu hii ikiisha, kijusi huwa na urefu wa centimita 10 na gramu 28.
Awamu ya pili
  • Viungo vinaendele kukua na kijusi kwa wakati huu kinakua upesi
  • Nyushi na kucha zinaota
  • Kijusi kinaanza kusonga, kurusha mateke, kulala, kuamka, kumeza, kusikiza na kukojaa
  • Ngozi ya mwili kwa wakati huu imejikunja na huwa na nywele
  • Kujusi huwa na urefu wa centimita 30 na huwa na uzito wa kilo moja awamu/kipindi hiki kikikamilika
 
Awamu ya tatu
  • Nywele zilizo mwilini zinatoweka
  • Mifupa ya mwili inakuwa migumu lakini ya kichwa huendelea kuwa ya kunyumbuka/kukunjikana
  • Kijusi hukaa
  • Awamu hii ikikamilika, kijusi huwa cha centimita 50 na uzito wa kilo 3-4
 
Jihusishe na ujifunze jinsi unavyoweza kukaa kwa afya wakati wa mimba. Unaweza kumuuliza daktari wako maelezo ili kumpa mwanao msingi bora wa maisha.Yanayoweza kumdhuru mtoto tumboni
 
MIMBA ni kawaida na ni kitu cha asili. Kila mwaka mamilioni ya wanawake hubeba mimba. Ubora wa mimba utategemea na ufahamu wa mwanamke katika kuyaweka mazingira bora kwa kiumbe kinachokuwa (fetus).
Kufahamu matatizo yanayoweza kumdhuru mtoto tumboni kuna wawezesha wajawazito kuwa waangalifu zaidi kuliko kutofahamu lolote. Hii hasa husababishwa na ule udhaifu alionao mtoto kwani hutegemea mama yake kwa karibu asilimia 98. Hivyo basi kitoto kinachokuwa tumboni chaweza kusumbuliwa au kumdhuru kiakili au kimwili kilingana na kiwango alichoumia mwanamke huyo. 
Chakula bora na mazoezi ni muhimu kwa wote yaani mama mtarajiwa na mtoto atakaezaliwa. 
Miongoni vya vitu vinavyoweza kumdhuru mtoto tumboni ni magonjwa, caffaine, madawa ya kulevya, pombe,sigara, mionzi hasa isiyoyalazima. 
Asilimia kuwa ya madawa anayokunywa mjamzito hupitia kwenye "Placenta' na kuingia kwenye mishipa ya damu ya mtoto. Ujauzito una vipindi mbalimbali kufuatana na ukuaji wa mtoto. Si madawa yote hayafai kwa wajawazito na si madawa yote yanafaa wakati wote wa ujauzito. Madawa mengine hayafai miezi ya mwanzo na mengine hayafai miezi ya mwisho ya ujauzito. Iwapo yatanywewa bila kuzingatia hilo, mtoto aliyetumboni anaweza kudhuriwa bila kufahamu. Mjamzito asinywe dawa bila ushauriwa na daktari. Hata kama unaumwa na kunadawa za mtu mwingine, kwanza shauriana na daktari au mtaalamu wa dawa. Madawa ya kulevya ndio hatari zaidi. Wajawazito washauriwe kuacha kabisa utumiaji wa madawa haya haramu. 
Caffeine hupatikana katika kahawa, chai, coka cola na chokoleti. Madini haya japo huweza kuwadhuru hata watu wakubwa huweza pia kusababisha madhara kwa mtoto aliye tumboni. Wajawazito washauriwe kupunguza unywaji wa kahawa, chai, chokoleti au vinywaji na vyakaula vyenye "cola". Iwapo mazoea yameshindikana kuachwa basi kahawa au majani ya chai yaliyotolewa caffein yatumiwe (decafeinated coffee). 
"Tetekuwanga" ni ugonjwa unaowapata hasa watoto wadogo. Lakini yawezakutokea kumpata mtu mzima. Ugonjwa huu huweza kumdhuru mama na mtoto aliyetumboni. Mjamzito atakapoumwa tekekuwanga, anaweza kuzaa mtoto mwenye mtindio wa ubongo, kipofu, mwenye matatizo ya ngozi na aliyedhoofu. Iwapo hujapata sindano ya kinga, ni vizuri kumwona daktari mapema kabla ya tatizo lolote kukuanza. 
Sigara na uvutaji wake huwathiri watumiaji wake popote walipo. Mjamzito pamoja na kujidhuru yeye mwenyewe, humdhuru pia mtoto aliye tumboni. Wajawazito walio wavutaji huweza kuzaa mtoto mwenye uzito wa chini "kabichi" au"njiti', mtoto pia anaweza kupata matatizo ya mapafu "pneumonia" na kudhoofu afya kwa ujumla. 
Vile vile hata kma mjamzito havuti sigara, wanafamilia wengine wanaweza kumdhuru iwapo watakuwa wanavuta. Wanawake na watoto wengi hudhururiwa na moshi wa sigara ndani ya majumba yao. Hasa pale baba anapomaliza nusu paketi akiwa ndani ya nyumba yao! Kina baba msiyachafue mazingira ya nyumbani iwapo hamuwezi kabisa kuacha uvutaji. 
Pombe ni sumu ya viungo vinavyokuwa. Inaponywewa na mjamzito huingia katika mishipa ya damu ya mtoto kupitia "placenta". Pombe hudhuru viungo dhaifu vya mtoto vinavyokuwa. 
Watoto wanaozaliwa na wanawake walevi huwa na tatizo la ukuaji dhaifu wa ubongo hivyo kuwafanya wasiwe na akili "nzuri". Uzito mdogo wakati wa kuzaliwa, matatizo ya moyo,figo na macho, matatizo ya mifupa pia huweza kuwapata watoto hawa. 
Hata kiasi kidogo cha pombe kinatosha kabisa kuwa na madhara kwa mtoto aliye tumboni. Ni vizuri kuacha kabisa vinywaji hivi iwapo unampenda atakayekuwa mwanao siku zijazo. Kwa wajawazito achana na marafiki walevi na kuwa mkali kwa mume au jamaa atakayekuletea zawadi ya pombe. Usitembelee kabisa sehemu zinazouzwa pombe, wala usikodolee macho matangazo ya pombe. 
 

Post a Comment

POPULAR POST

 
Top