Msanii wa filamu nchini Elizabeth Michael aka Lulu amesema vijana wanatakiwa wawe mstari wa mbele katika kujikinga na maambukizi ya virusi vya Ukimwi.
Akizungumza na mwandishi wetu jana katika usiku wa Red Ribbon Fashion Galla
iliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam, Lulu alisema siku ya
Ukimwi duniani inatukumbusha kuangalia tumetoka wapi na tunakwenda wapi
na kuangalia wangapi wamepoteza maisha kwaajili ya gonjwa la Ukimwi.
“Najumuika na Watanzania leo ,siku ya Ukimwi duniani ambayo hufanyika
kila mwaka, kwa kuangalia wangapi wamepoteza maisha, pamoja na
kuwahamasisha zaidi vijana Wakitanzania kutumia kinga ili kupunguza
maambukizi ya virusi vya Ukimwi ambavyo vinapoteza nguvu ya Taifa,”
alisema Lulu.
Pia Lulu alisema amekuwa akipima Ukimwi mara kwa mara ili kuangalia
afya yake,huku akiwashauri vijana kwenda kupima ili kujua afya zao.
“Nimekuwa nikipima HIV kila mara katika hatua za maisha
yangu,kuangalia kuhakikisha najiweka katika usalama wa afya yangu,pamoja
na kupanga matarajio ya maisha.Sio kuwa ukipima ukagundulikana una HIV
utashindwa kupanga malengo yako hapana! ukipata ushauri nasaha, ukajua
uishi vipi kwa kuboresha afya yako, maisha yataendelea kama kawaida.
Kwahiyo kinachotakiwa vijana ni kujua afya zetu mapema”
Post a Comment