Dawa au vifaa vya uzazi ni baadhi ya taratibu zinazotumiwa kuzuia mimba kutungwa. Ikiwa msichana au wanamke atafanya mapenzi pasi na kutumia mojawapo ya mbinu hizo basi, kuna uwezekano wa theluthi moja kwamba atapata mimba.
Hata hivyo aina yoyote ya kuzuia mimba utakayoichagua ni lazima itumiwe kama ilivyoagizwa, ili kuleta matokeo ya hakika.
Baadhi ya njia hizo kama vile kutumia kondom wakati wa ngono, pia kwa
kiasi fulani humpa mtu kinga dhidi ya maambukizo ya virusi vya HIV, na
magonjwa mengine yanayoathiri afya ya uzazi.
Kwa vile mbinu za kuzuia uzazi ni za aina tofauti tofauti, ni muhimu
basi uchague kwa makini ile inayokufaa. Utapata usaidizi wa kitaalam
kama utashauriana na daktari wako, au pata usaidizi katika kituo cha
kwenu cha upangaji uzazi, au kituo cha vijana.
Hivi ni vifaa au dawa zinazotumiwa kwa minajili ya kuzuia mimba kutungwa wakati wa kufanya ngono.
Kuna zile zinazotumiwa kwa mda mfupi na nyengine kwa mda mrefu. Nyengine
hufanya kazi papo hapo na nyengine huitaji maandalizi ya mda. Kondom au
tembe maalum ndizo njia bora zinazojulikana zaidi za kuzuia mimba.
Pia kondom zina manufaa bora zaidi zinapotumuwa kwani mbali na kuzuia
mimba zinapotumika kama inavyopaswa zinaweza pia kumkinga mtu
asiambukizwe vurusi vya HIV, na magonjwa mengine ya zinaa.
Tuangalie kwanza vifaa vya kuzuia mimba.
Moja ya mbinu bora na rahisi za kuzuia mimba, ni kuweka kizuizi, kwa
lengo kuwa mbegu ya mwaname na ile mwanamke zisikutane. Kwa maana hiyo
kifaa maalum kinaweza kuwekwa katika njia inayotumiwa na mbegu ya kiume
ndio isilifikie yai la mwanamke. Baadhi ya vifaa hivi (hasa kondom) pia
vinaweza kukinga kuambukizwa virusi vya Ukimwi, na magonjwa mengine ya
kuambukizana kupitia ngono.
Kuna aina kadhaa za vifaa vya kuzuia mimba. Kondom za wanaume na zile za
wanawake ndio vifaa vinavyofahamika zaidi, hata hivyo kuna pia vifaa
vyenginevyo viitwavyo diaphragm na caps kwa kimombo ambavyo vinaweza
kutumiwa na wanawake.
Kondom
za wanaume: Hivi hutengenezwa kutokana na aina maalum ya mpira uitwao
latex, au plastiki nyembamba. Kondom ya mwanaume huvaliwa kwenye uume
iliyosimama, tena kabla ya uume kuingizwa ukeni. Ikitumiwa kama
inavyotakikana inakadiriwa kuzuia mimba kwa asilimia 98.
Kwa kawaida kondomu hupatikana kwenye vituo au kliniki za upangaji uzazi, kwenye maduka ya madawa au hata maduka ya kawaida.
Kondomu za wanawake: Halkadhalika hutengenezwa kwa mipira laini ya latex
au plastiki nyembamba maalum. Huvaliwa ndani ya uke, huku sehemu
iliyowazi ikichomoza nje kidogo. Kwa kawaida kondom za wanawake ni
ghali, na pia utendaji kazi wake unakadiriwa kuzuia mimba kwa asilimia
95.
Aina nyenginezo na vifaa vya kuzuia mimba huwa hazipendekezwi kwa vijana lakini ni vyema kuvijua.
Kuna aina nyenginezo za vifaa vya kuzuia mimba viitwavyo diaphragms na
caps. Hivi hutengenezwa kutokana na kitu kiitwacho silicone au mpira
laini maalum. Vikiwekwa ukeni hutumika kama vizibo vya kuzuia mbegu za
mwanamme kupenya hivyo basi haiwezi kukutana na yai la mwanamke.
Kwa kawaida caps ni ndogo kuliko diaphragms lakini kwa vile wanawake pia
wana maumbo tofauti, ni sharti upate saizi utakayokutosha. Hapa ni
sharti upate usaidizi wa daktari wako, au muuguzi, kuiweka.
Inapowekwa mahali pake ndani ya uke, iwe diaphragm au cap, huziba
kilango cha mfuko wa uzazi hivyo basi mbegu ya mwanamme haitapatanafasi
ya kupita. Ukishaonyeshwa na daktari jinsi ya kuipachika, baadae unaweza
kuipachika mwenyewe kabla ya kufanya mapenzi.
Kwa matokeo bora zaidi, diaphragms na caps hutumiwa pamoja na dawa
iitwayo (spermicide) ambayo huuwa mbegu za uzazi za mwaname. Hapo
diaphragms au caps humpa mwanamke kinga dhidi ya mimba kwa asilimia kati
ya 92 na 98.
Hata hivyo itachukua mazoezi ya muda ili kuvitumia itakikanavyo. Wakati
mwengine pia hutumiwa na gel yake maalum lakini bado havina hakikisho la
asilimia moja kuzuia mimba.
Faida yake nyengine ni kuwa, kwa kiasi fulani, vinaweza kukinga dhidi ya
magonjwa ya zinaa na saratani ya (cervix) lango la nyumba ya uzazi.
Ikiwa wewe hutumia vifaa kama diaphragms au caps, au hata kondom, ni
vyema kujipangia mapema ndio usikose akiba, ndio haitakuwa karaha
kuvitafuta pale unapovihitaji.
Mbinu nyingine za kuzuia mimba
Kuna chembe chembe za kimaumbile, zinazojulikana vyema kama homornes
ambazo hutumiwa kutengeneza tembe au chanzo ya kuzuia mimba.
Chembe chembe hizi kwa jina maalum progestogen yaani mchanganiyko wa
oestrogen na progestogen, huingizwa mwilini mwa mwanamke kwa mpangilio
na kiwango maalum ili kuzuia mimba kutungwa.
Hufanya kazi kwa namna hii:
Kwa kuzuia ovari kuangua mayai Kwa kuzuia mbegu za mwanamme kulifikia
yai (kwa kufanya majimaji ua ukeni kuwa mazito na kunata hivyo kuzuia
mbegu ya mwanamme kupenya) Kwa kulizuia yai kujipachika kwenye kiota cha
nyumba ya uzazi.
Tembe mchanganyiko - huwani kidonge cha dawa kilichotengenezwa kwa
mchanganyiko wa chembe chembe za oestrogen na progestogen. Hii huzuia
mimba kwa njia zote tatu tulizozitaja hapo juu na ikitumiwa
itakikanavyo, vinategemewa kuzuia mimba kwa asilimia 99.
Tembe ni rahisi kutumia - Mradi tu unakumbuka kumeza vidonge kulingana
na maagizo. Wakati mwengine pia huifanya hedhi, kupungua na kupunguza
pia maumivu wakati wa hedhi.
Lakini
athari zinazoandamana na utumiaji wa vidonge hivyo ni pamoja na
kuchafukwa na moyo, kuongezeka unzani, na athari mbaya zaidi ni iwapo
itatokea hali ya kuganda kwa damu kwenye mishipa ya kupitisha damu.
Vidonge vya Progestogen pekee (POP) -Aina hii ya Tembe huitwa pia “mini
pill” na huwa ina chembe chemba za progestogen pekee. Huzuia mimba kwa
njia kama zile zile zinazozuia tembe za mchanganyiko, na ina utendaji
kazi wa kati ya asilimia 96 na 99. Hata hivyo kama una uzani wa zaidi ya
kilo 70 uwezo wake wa kuzuia mimba hupungua
Faida kuu ya kutumia vidonge hivi ni kwamba vina athari ndogo za kiafya.
Lakini tatizo ni kuwa ni sharti tembe imezwe wakati ule ule kila siku ,
kama umechelewa basi isipitishe zaidi ya masaa matatu.
Sindano - Hii ni chanjo ya kuzuia mimba inayotengenezwa na chembe chembe
hizo hizo za homoni ya progestogen. Tofauti na tembe, ambazo ni sharti
kumeza moja kila siku, sindano pindi inapodungwa inakupa kinga dhidi ya
mimba, kwa mda wa kati ya wiki nane hadi 12 kuambatana na aina
inayotumiwa.
Hudungwa takoni, na dawa kuingizwa ndani ya mishipa ya damu na ina uwezo wa kuzuia mimba kwa asilimia 99.
Faida kuu ya njia hii ya sindano, ni kwamba hutakuwa na wasiwasi wa
kupata mimba unapofanya ngono, kwa mda wa angalau wiki nane au 12.
Lakini pia ina athari zake - ni kwamba huenda dawa hii ikavuruga
mpangilio wako wa kawaida wa kupata hedhi, au ukatoka hedhi kiwango
kisicho cha kawaida cha damu, au kwa mda mrefu, au hedhi ikapotea
kabisa. Pia inaweza kusababisha kuongezeka uzani.
Homoni au Vidonge vya kupachika chini ya ngozi Hapa dawa kama ile ile ya
tembe au chanjo, hutengenezwa na kuwekwa kwenye kifaa cha plastic mfano
wa kijiti cha kiberiti. Hupachikwa ndani ya ngozi chini ya kwapa kwa
kufanyiwa upasuaji mdogo.
Hii ni njia ya mda mrefu ya kuzuia mimba. Inaaminika kuzuia mimba kwa
aslimia 99 na inaweza kufanya kazi kwa mda wa hadi miaka mitatu.
Kuna aina nyenginezo za upangaji uzazi ambazo, ingawa kwa hali ya kawaida hazipendekezwi kwa vijana, si vibaya kuzijua.
Kitanzi au koili, ambacho kwa lughaya kitaalam kinajulikana kama
Intra-uterine device au IUD hutengenezwa kwa plastiki na shaba, na
hupachikwa kwenye mfuko wa uzazi na daktari au muuguzi.
Vitanzi
huanza kufanya kazi pindi kinapopachikwa. Hufanya kazi kwa njia mbili
kuu. Kwanza, kwa kuzuia mbegu za kiume kutangamana na yai, na pili
kuzuia yai kukubaliwa kujipachika ndani ya mfuko wa uzazi.
Kitanzi au koili kinakadiriwa kuzuia mimba kwa asilimia 98 na 99. Na
pindi kikitolewa asili ya uwezo wa wanamke wa kushika mimba anapofanya
ngono, unarudi vilevile.
Hata hivyo moja ya matatizo ya kitanzi ni kwamba vinaweza kuifanya hedhi
yako kuwa nzito (damu kutoka nyingi) na pia huenda ukapatwa na maumivu,
mara nyengine inaweza kutoka mahali kilipowekwa na kusukumwa nje ya
mfuko wa uzazi.
Hivyo ni vyema kumuona daktari mara kwa mara ili kama imechomoka, ipachikwe tena vyema.
Njia asilia ya mpango wa uzazi.
Njia hii inahitaji makini sana kuitumia. Kwani inafanya kazi tu ikiwa
wanamke anafanya mapenzi tu wakati ule ambao kiasilia hawezi kushika
mimba.
Hii inawezekana kwa kutayarisha tarakimu za siku za hedhi, na kupima
hali ya joto la mwili. Njia hii inahitaji uangalifu na uzoufu mkubwa –
Kwa vile ni ya kubahatisha haipendkezwi kwa vijana ambao hawako tayari
kupata mtoto.
Kwa bahati mbaya watu wengi hudhani kwamba kutoa uume kutoka ukeni,
pindi tu kabla ya kufikia kilele cha kumwaga manii, ni moja ya njia za
kuzuia mimba.
La sivyo kwani mara nyingi mbegu za kiume hutangulia kutoka hata kabla
kufikia kilele katika hali ya kufanya mapenzi. Hivyo basi hata ukitoa
uume huenda umeshachelewa!
Vasectomy au Tubuligation,
Hii ndiyo njia pekee ya kudumu ya kuzuia mimba.
Vasectomy
ni njia ya kumfanya mwanamme asiwe na uwezo wa kutunga mimba ilhali
Tubuligation ni njia ya kumfanya mwanamke asiwe na uwezo wa kushika
mimba. Hii inafanyika kwa njia ya upasuaji mdogo.
Mwanamme
anafanyiwa upasuaji kwa kukata vibomba vinavyopitisha mbegu za kiume
kutoka kwenye makende hadi kwenye uume. Upasuaji huu kwa mwanamke
unahusisha kukatwa au kuzibwa kwa vibomba vinavyopitisha mayai kutoka
kwa ovari hadi kwenye mfuko wa uzazi.
Baada ya upasuaji huu, ni
vigumu mwanamke au mwanamme kurudishwa tena katika hali ya mwanzo ya
kuweza kuzaa, kwa hivyo njia hii inatumiwa tu kwa sababu za kimatibabu
au ikiwa mhusika amefikia uamuzi wa hakika kwamba hataki tena kupata
watoto (zaidi).
Kitanzi cha Intra uterine system au IUS -Hiki
nacho kimetengezwa kwa plastiki, yenye muundo wa T kikiwa na chechembe
za homoni ya progestogen ndani. Kinaweza kupachikwa ndani ya mfuko wa
uzazi na daktari au muuguzi.
Kitakapopachikwa, progestogen pole
pole huingia ndani ya mwili, na kuzuia mimba katika njia ile ile kama
vinavyozuia tembe. Kinaweza kutumika kwa mda wa miaka 5, na kinakadiriwa
kuzuia mimba kwa asilimia 99.
Kitanzi cha IUS ni kizuri kwa wale
walio na matatizo ya maumivu wakati wa hedhi, kwa sababu kinapopachikwa
(ingawa wakati wa kupachikwa huenda ukapata maumivu kidogo) baadaye
husaidia kupunguza hedhi au hata kuisitisha kabisa, kutokana na homoni
hizo za progestogen.
Madhara ya njia hii nayo ni kama, kuongeza
uzani, kuumwa na kichwa, kutokwa na damu kusiko na mpango, na mabadiliko
ya majira ya hedhi. Pia inaweza kuchopoka, hivyo itabidi kumwona
muuguzi au daktari kila mwezi kuhakikisha kiko sawa.
Post a Comment