Mama mmoja baada ya kukaa kwa muda mrefu bila kushika mimba, aliamua kwenda kwa mchungaji mmoja ambaye alitoka nchi ya mbali na kuja pale mtaani kwao akiwafanyia watu miujiza mbalimbali kupitia maombi yake na mama akaomba kuombewa ili apate mtoto.

Mchungaji yule alimfanyia ibada fupi na miezi michache baadae yule mama alibahatika kupata mimba na kuibeba kwa miezi tisa kisha akajifungua salama mtoto wa kiume.

Mama yule aliendelea kumtunza mwanae kwa kumnyonyesha ingawa kila alipomnyonyesha mtoto yule mama aliishiwa nguvu na kulala kwa muda kabla ya kuamka na kuendelea na kazi.

Jambo lile lilimshtua sana mama lakini akafikiri labda ni tatizo la kawaida kwani hakuwahi kuwa na mtoto.

Akaamua amwanzishie kumpa maziwa na kumwomba msichana wake wa kazi kuwa awe anampa maziwa pindi yeye yupo kazini na akawa akinunua maziwa lita tatu ili yaweze kukaa kwa siku tatu.

Maajabu ni kwamba lita tatu ziliisha kwa siku na mama kwa kuwa alipenda kwenda na bajeti hivyo alimkaripia msichana wa kazi na kumpiga sana kwa kumaliza maziwa lita tatu kwa siku.

Binti alilalamika sana na kusema mama huwa nayachemsha na kuyaacha mengine kwenye sufuria kisha kidogo namnywesha mtoto na ninaendelea na kazi kabla ya kuja kuangalia na kuona mazima yameisha kwenye sufuria.

Mama hakuamini na binti akaamua kuweka mtego ili aone kama ni majirani wanamfanyia visa au kuna kitu ambacho hunywa maziwa yale.

Siku iliyofuata baada ya kumnywesha mtoto maziwa akamlaza kitandani karibu na ile sufuria ya maziwa na kujificha nje akiangalia kila kilichokuwa kikiendelea mle ndani.

Mara akaona mtoto yule anabadilika na kuwa joka kubwa na kunywa yale maziwa na kisha kurudia umbo lake la mtoto.

Binti akakimbia mpaka kwa mama na kumwambia ingawa mama akawa mbishi kuamini na siku ya pili wakafanya kwa pamoja na baada ya dakika chache mama akamshangaa mwanae wa pekee akibadilika na kuwa nyoka.

Mama alipiga kelele na kwenda kwa mchungaji na mchungaji akasema wakamlete mtoto na alipoletewa yule mtoto, mchungaji akamkumbatia na mtoto yule kupotelea kifuani kwake.

Mama yule aliondoka na kwenda kibandani mwake ili afunge na kurudi nyumbani kabla ya kushangaa kuona kuwa yule nyoka kaja kibandani kwake ..... Akakichoma kibanda chake na kwenda kanisa lake la mwanzo ambako alifanyiwa maombi na kutolewa vitu vya ajabu tumboni mwake na kutaapishwa maji aliyokuwa akinyweshwa na yule mchungaji feki.

Sasa hivi yule mama kamrudia Mungu wake na ana mme na mtoto mmoja na yule mchungaji akiyempa yule mtoto nyoka alikimbia na haijulikani aliko.

Mama yule kila akisoma amri ya Mungu ya kwanza kwetu wanadamu hulia sana na kumwomba Mungu amsamehe kwa kupotoka kwake na amri hiyo yasema, " Mimi ndimi Bwana Mungu wako Usiabudu miungu mingine ila mimi"

Nami nakuombea rafiki yangu hata pale unapoandamwa na matatizo ya dunia, mapito magumu au kukosa furaha na amani katika maisha kamewe Usiabudu miungu mingine.


Post a Comment

POPULAR POST

 
Top