A. MKAGUZI MSAIDIZI WA UHAMIAJI (Nafasi 70)
- SIFA ZINAZOHITAJIKA
- Awe na Shahada ya Kwanza au Stashahada ya Juu kutoka Vyuo Vikuu vinavyotambuliwa na Serikali katika fani zifuatazo:
- Awe na umri usiozidi miaka 35
- MAJUKUMU NA KAZI ZA KUFANYA
- Kusimamia doria sehemu za Mipakani, Bandarini, Vituo vya Mabasi, Treni na sehemu zenye vipenyo vya kuingia na kutoka nchini vikiwemo vya majini
- Kusimamia shughuli za upelelezi, kuandaa Hati ya Mashitaka na kuendesha mashitaka
- Kutoa na kupokea fomu mbali mbali za maombi ya Hati za Uhamiaji
- Kufanya Ukaguzi wa Mwanzo wa Maombi mbalimbali
- Kuagiza ufunguaji wa Majalada ya watumiaji
- Kupokea na kukagua Hati za Safari, Fomu za Kuingia na Kutoka Nchini
- Kuidhinisha malipo mbalimbali ya huduma za Uhamiaji kwa wanaostahili
- Kutunza kumbukumbu za ruhusa za watu wanaoingia na kutoka nchini
- Kukusanya, kusimamia na kutunza takwimu za Uhamiaji na Uraia
- Kuandaa majibu ya maombi yote ya huduma za uhamiaji yaliyokubaliwa au kukataliwa
1. SIFA ZINAZOHITAJIKA:
- Awe amehitimu Kidato cha Sita na kufaulu
- Awe na umri usiozidi miaka 30
1. SIFA ZINAZOHITAJIKA:
- Awe amehitimu Kidato cha Nne na kufaulu
- Awe na umri usiozidi miaka 25
- Cheti cha Ufundi Stadi (Full Technical Certificate) kwenye fani ya Umeme na Mitambo
- Cheti au Stashahada ya Uhaziri (Certificate or Diploma in Secretarial Studies) kutoka Chuo kinachotambulika na Serikali
- Cheti au Stashahada ya Kutunza Kumbukumbu (Certificate in Records Management) kutoka Chuo kinachotambulika na Serikali
- Cheti au Stashahada ya Takwimu (Certificate or Diploma in Statatistics ) Kutoka Chuo kinachotambulika na Serikali.
- Cheti au Stashahada ya Vyombo vya Majini (Certificate or Diploma in Marine Transportation and Operations) kutoka Chuo kinachotambulika na Serikali
- Cheti au Stashahada katika fani ya Uchapaji (Printing)
- Ujuzi na Elimu ya Kompyuta na Uandishi mzuri utazingatiwa
- Cheti cha Ufundi Makanika,Kozi ya juu ya Udereva na Leseni ya Udereva Daraja C
- Kufungua, kupanga na kutunza majalada ya huduma mbalimbali za Uhamiaji
- Kuandika Hati mbalimbali za Uhamiaji
- Kufanya doria sehemu za Mipakani, Bandarini, Vituo vya Mabasi, Treni na sehemu zenye vipenyo vya kuingia na kutoka nchini vikiwemo vya majini.
- Kusindikiza watuhumiwa wa kesi za Uhamiaji Mahakamani pamoja na wageni wanaofukuzwa nchini
- Kufanya ukaguzi kwenye mahoteli, nyumba za kulala wageni na sehemu za biashara.
- Kuchapa au kuandika kwa kompyuta barua au nyaraka mbalimbali zinazohusu kazi za kila siku za Uhamiaji.
- Kufanya matengenezo/ukarabati wa mitambo na vitendea kazi vya Uhamiaji
- Kuandaa na kutunza takwimu za huduma mbalimbali za uhamiaji
- Nakala za vyeti vya kuhitimu masomo kwa mujibu wa sifa zilizotajwa
- Nakala ya Cheti cha Kumaliza Elimu ya Msingi
- Nakala ya Cheti cha Kuzaliwa
- Picha mbili (Passport Size)
- Barua ya Utambulisho kutoka kwa Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa
Maombi yote yapitie posta na barua za maombi ziandikwe kwa mkono.
- Maombi ya nafasi ya Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji yatumwe kwa:
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI,
S.L.P. 9223, DAR ES SALAAM
- Maombi ya nafasi ya Koplo wa Uhamiaji na Konstebo wa Uhamiaji yatumwe kwa:
S.L.P. 512, DAR ES SALAAM
Mwisho wa kutuma maombi kwa nafasi zote ni tarehe 27/02/2014
Post a Comment