Basi msomaji wa Blog hii leo
nimeona niangalie kwa upana zaidi swala zima la hasira, hali ambayo binadamu
wengi hukabiliana nayo mara kwa mara, basi bila kupoteza muda tupa macho hapo
chini uone nini cha kufanya ili upunguze hasira zako.
1. Jaribu kuelewa ni kwanini umekasirika.
Ni muhimu ukaelewa kwamba umefikia hatua ya kuweza
kukasirika.Kama hali au mtu fulani akikukasirisha, nenda kazungumze na mtu
unaye muamini anaweza akawa rafiki wa karibu, daktari wako, wanasaikorojia au
watoa ushauri nasaha wanaweza
kukusikiliza na kukusaidia nini cha kufanya.
2. Jaribu kupumzika na kutuliza mawazo.
Kupumzika kunaweza kuweka mpangilio mzuri wa ufikiri
kichwani.Kupumzika kunaweza kukawa ni matembezi mafupi au kujiweka katika
mazingira tulivu yasiyo na kelele au bugudha ya aina yoyote ile.Ukiwa huko
matembezini ama sehemu tulivu, unaweza ukaangalia filamu, ukasoma kitabu,
ukasikiliza musiki, ukaoga au kuogelea.Ni muhimu kila siku ukatunza muda
kwaajiri ya kupumzika. Chagua kitu chote ambacho utafurahia kukifanya ufikapo
muda huo.
3. Fujo sii njia nzuri ya kumaliza hasira.
Wakati mwingine mtu anaweza akakukasirisha sana,
kitu ambacho kitakusababisha umvagae/ umvamie na kuanza kupigana.Mara nyingi
kuchukua uamuzi wa haraka na kutamka au kumvagaa mtu, hujaribu kuonyesha kile
kilichopo ndani ya moyo wako kwa wakati huo, kitu ambacho ni hatari sana!! na baada ya hapo
utakuta ukijiuliza aaah!! ni kwanini nimefanya hivyo?
Kuwa tayari kuzuia hali ya ugomvi wakati ukiwa na hasira,
andika chini list ya hali, Watu au vitu vinavyo kufanya ufanye fujo.Baada ya
kuandika vitu vyote ambavyo mara nyingi hukusababisha kukasirika, angalia sasa
njia ya kuepukana navyo.Pia kuna baadhi ya watu ambao wanaweza kukusaidia jinsi
ya kuepukana na hisia za kuvamia watu wakati ukiwa na hasira.
1. Unatakiwa kuelewa kuwa kila mtu maishani
mwake ana matatizo yake.
Sababu za wewe kutokuelewana na mtu mwingine ni nyingi,
kwamfano itakuwa ni vigumu kuelewa anachokiwaza mtu mwingine kuhusu jambo
fulani.
Lakini unatakiwa kujaribu kufikiri je watu wengine
wanafikiri vipi kuhusu jambo fulani kabla hujachukuwa hatua.Jaribu kusikiliza
ushauri wa watu lakini baada ya hapo usiharakishe kuutumia ushauri huo,
kaachini tafakari, chuja na chukuwa hatua.
Sii kila ushauri huwa ni mzuri, kwamfano mwingine huchochea
ugomvi, mauwaji, taraka, kuvunja mahusiano na mwisho wa siku unakuta unaishia
pagumu zaidi.
Niwachache wanaweza kufurahia mafanikio yako, hivyo utakapo
hitaji ushauri tu kosa, wanakuwa wamepata nafasi ya kukusambaratisha “take
care”!!.
2. Suruhisha migogoro yoyote inapotokea.
Migogoro ambayo haijapatiwa ufumbuzi huweza kuleta
mkanganyiko na challenge kubwa katika maisha.”Mzaha mzaha hutumbukia usaha”
mbaya zaidi hali hiyo inaweza kusababisha mshituko, kukosa usingizi, magonjwa,
kudolola kwa mahusiano, fujo na kuvunjika kwa familia. Mfano mzuri ni moja ya
filamu ya kibongo ambayo kwa bahati mbaya siwezi kuikumbuka jina lake.
Lakini ilikuwa ni
mgogoro mkubwa sana kati ya mume na mke ndani ya
nyumba, hadi kufikia hatua ya kutaka kugawana mali zilizomo ndani ya nyumba.
Lakini rafiki wa mume ndiye aliyeweza kuinusuru vyema ndoa
hiyo iliyokuwa kati kati ya mikono ya shetani, alichofanya alitazama wapi uzito
wa mgogoro ulipotokea alafu akadili nao huku akijaribu kutoa mifano
mikubwa ya matatizo aliyokwisha
kabiliana nayo, nahiyo ilisaidia kumuonyesha yule bwana kuwa tatizo alilonalo
ni dogo sana,
hivyo jamaa akarudi kuwa mpole ndani ya nyumba na mambo yakasonga.
3. Amua migogoro kadri ya unavyoweza.
Kama kuna mgogoro kwa mtu
mwingine ni rahisi kuwapunguzia hasira wawili hao. Nirahisi kwa mtu kusuruhisha
iwapo umekuwa ukitazama tukio zimima wkati linatokea.Nivyema ukiamua
kusuruhisha ukajitosa kiukweli, kwamfano
unweza ukatumia simu kumpigia kila mmoja nakuzungumza naye na kuona kama wanania ya kupata mwafaka?
Unaweza kuwaambia jinsi ulivyo sikitishwa na mgogoro huo, na
pia unaweza ukatafuta mtu mwingine mwenye busara ambaye ataweza kukupiga tafu
huku akijaribu kutoa mifano harisi kwa mfano ting’a zozote zile alizowahi
kukumbana nazo.
Basi mpendwa msoma
ukurasa huu haujaishia hapa bali ndo kwanza unaanza!! Usikose ukurasa unaokuja
coz unakuhusu wewe zaidi katika maisha yako ya kilasiku, pamoja sana!!!
Post a Comment