Watu wanne wa familia moja wamekatwa na polisi katika kata ya Busega, mkoani Simiyu baada ya kukutwa wakilima huku wakiwa uchi. Kaimu Kamanda ya Polisi mkoani Siminyu Venance Kimario amedhibitisha kutokea kwa tukio hilo baada ya polisi kufahamishwa na raia mwema katika kijiji cha Bushigwamala kilichopo Kivukoni wilayani Busega. 

Waliokamatwa ni baba mzani Makoye Gamoge (42), mama mzani Neema Kugela (31), mtoto wao wa kiume Juma Makoye (15) na mtoto wao wa kike Esther Makoye (12). Watoto hao wanasoma katika shule ya msingi ya Bushigwamala. Wote wanne hawakukimbia baada ya kuwaona polisi kwenye mida ya saa kumi na mbili za asubuhi. Waliendelea kulima huku wakiimba bila kuogopa uwepo wa polisi shambani hapo mpaka pale polisi walipowaamuru waweke majembe yao chini.

Kwa mujibu wa RPC baba mzani Gamoge amedai kuwa kitendo cha mtu kulima wakati akiwa uchi ni sehemu ya tamaduni za Wanyantuzu ambao ni sehemu ya kabila la Wasukuma na madhumuni yake ni kuleta mvua za kutosha na hivyo mavuno mazuri. Amesema kuwa walikuwa wanalima uchi kutoa heshima kwa nasaba zao. Gamoge aliongeza kwa kuwambia polisi kuwa familia yake ilishauriwa na mganga wa kienyeji aliyewahakikishia "mapinduzi ya kijani" kama kama wangefuata ushauri wa kulima mapema asubuhi huku wakiwa uchi. 
sasa hata kama ndio mira zetu lakini kiimani ya watu wasio jua utamaduni wao tukio hili hufananisha na matukio ya kishirikina. 

Post a Comment

POPULAR POST

 
Top