WATU zaidi ya 25
wajeruhiwa vibaya katika ajali iliyotokea jana baada ya gari walilokuwa
wakisafiria aina ya Toyota Costa kutoka Mbozi kuelekea Mbeya kupinduka
katika eneo la Senjele wilayani Mbozi Mkoa wa Mbeya.
Ajali hiyo ilihusisha gari aina ya Costa lenye namba za usajili T 336 CJY ambalo lilipinduka baada ya kumshinda dereva wakati akijaribu kulikwepa gari linguine aina ya Suzuki lenye namba za usajili T 327 ARZ.
Kwa mujibu wa baadhi ya majeruhi walionusurika kwenye ajali hiyo walisema chanzo ni dereva kushindwa kulimudu gari la abiria baada ya kulikwepa gari dogo kutokana na kuwa na mwendokasi pamoja na mvua kubwa iliyokuwa ikiendelea kunyesha.

Baadhi ya majeruhi
walikimbizwa katika Hospitali teule ya Ifisi na wengine wakipelekwa
katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya kwa ajili ya matibabu zaidi.
Baadhi ya majeruhi wakitafuta mizigo yao mara baada ya kutoka ndani ya basi hilo
Baadhi ya abilia wakitaka kumpiga Dereva wagari ya aina ya Suzuki kuwa
yeye ndio alisababisha ajali hiyo kwa kuyumbayumba kwake barabarani
Post a Comment