REPPA PRINCE D’ANGOLA NJIANI KUJIONDOA WENGE MUSICA MAISON MERE ?
Ingawa bado hajatamka Rasmi, ila dalili zote zaonyesha kwamba Kijana PRINCE D’ANGOLA hana tena Mpangilio wakuendelea kushirikiana na Group WENGE MUSICA MM linalo ongozwa na WERRASON.
Palitokea na itilafu kadhaa iliopelekea kutoweka kwa maelewano kati yake na PAPY KAKOL, nusura watwangane Makonde . Kwa Bahati nzuri HERITIER WATANABE kaingilia kati na hali ya shwari ikarudi kama kawaida.
Ila kutokana na Purukushani hiyo, REPA PRINCE D’ANGOLA kaamua kuondoka kwahasira Jukwaani pale walipokuepo wakidumbwiza kwenye Parking ya GRAND HOTEL DE KINSHASA. na kusababisha SHOO ikatishwe kwa Mda.
Yasemekana chanzo cha Mzozo huo, ni Kitendo cha Reppa PRINCE D’ANGOLA kuonekana akishirikiana sana na Vijana wa QUARTIER LATIN ya KOFFI OLOMIDE pale alipopanda jukwaani nakuimbanao kwa pamoja siku ya Mazishi ya Mwanamuziki BABIA NDONGA CHOKORO.
WERRASON na Baadhi ya Viongozi wa Kamati kuu ya Group WENGE MM hawajaridhishwa kabisa na kitendo cha REPPA PRINCE D’ANGOLA. Ingawa wakati akiwa Jukwaani na Group la MOPAO MOKONZI, kamtupia sifa nyingi WERRASON .
Kwa Sasa kijana huyo mwenye Kipaji cha usanii Bado hajachukua Uamuzi wowote, ila kakiri kupokea Wito wa Mashabiki Wengi wakimhimiza aende kujiunga na FERRE GOLA!!!
Tunasubiria Jibu kutoka kwa Wasemaji wa Orchestra WENGE MUSICA MM, kwa kawaida CHIZI WA MFALME » WEWA SANKARA DE KUNTA » hua hachelewi kutoa maoni yake kwa Jambo lolote linalo husiana na WERRASON …