Baadhi
ya watu waliozungumza na mwandishi wa habari hizi Jumatano iliyopita
akiwemo mama wa marehemu, walisema kwa siku mbili hizo alizofanya kazi
hausigeli huyo alionekana kuwa na mambo ya kishirikina kwani asubuhi ya siku ya tukio aliamka akiwa amenyolewa nywele upande mmoja.
“Siku
hiyo ya Jumapili huyo mdada wa kazi aliamka akiwa amenyolewa nywele
upande mmoja, alipoambiwa amalizie zote alikataa akisema atanyoa baada
ya kutoka sokoni ambapo hakurudi tena,” alisema mama wa marehemu.
Hausigeli
aliyejulikana kwa jina moja la Ester (14) yupo matatani kwa madai ya
kumuua mtoto Arafat Allan (3) kwa kumnyonga shingo na kumpiga na kitu
kizito kichwani kisha kuutumbukiza mwili wake kwenye dimbwi la maji
machafu,
Mama wa Mtoto akiwa hospital |
Akizungumza
kwa uchungu, mama mzazi wa mtoto huyo, Zakia Peter ambaye amelazwa
katika Zahanati ya Kellen kutokana na mshtuko wa kifo cha mwanaye,
alisema siku ya tukio, hausigeli huyo aliyekuwa na siku mbili tangu
aanze kazi aling’ang’ania kutumwa sokoni saa mbili asubuhi ambapo
alimkubalia na kumuagiza mboga.
mwili
huo ulipelekwa katika Hospitali Teule ya Tumbi, Kibaha ambapo madaktari
waliufanyia uchunguzi na kubaini kuwa marehemu alinyongwa shingo na
kupigwa na kitu kizito kichwani hali iliyomsababishia mauti.
Jumatatu
iliyopita, siku moja baada ya tukio, hausigeli huyo alikutwa
akirandaranda stendi akiomba fedha za nauli ili arudi kwao Mbeya lakini
alikamatwa na kufikishwa kwenye kituo kidogo cha polisi.
Habari zinasema hali kwenye kituo hicho ilikuwa mbaya kufuatia baadhi ya wakazi wa eneo hilo kujaribu kukivamia ili wamuue mtuhumiwa huyo. Ilibidi mtuhumiwa ahamishiwe Kituo cha Polisi cha Tumbi, Kibaha.
Post a Comment