NewsImages/6008614.jpg
DONDOO
Madhara ya dawa
Kichefuchefu na kutapika,Upungufu wa damu,kuongezeka uzito,uhanithi na kukosa hamu ya tendo la ndoa.Matatizo katika ini na matiti kuwa makubwa.
Baadhi ya madaktari hutumia upasuaji wa kuondoa korodani kama njia ya kupunguza kiwango cha homoni hizi huzalishwa kwenye korodani. Hata hivyo tiba hii haifanyiki mara kwa mara.
Tiba ya Homoni
Hii ni aina ya tiba inayotumia dawa zinazopunguza kiwango au ufanyakazi wa homoni ya testosterone mwilini. Tiba ya Homoni hutolewa kwa wanaume walio katika hatua za mwisho za ugonjwa huu kwa nia ya kupunguza maumivu na kutibu dalili za ugonjwa.
Mengi yamesemwa kuhusu saratani za aina mbalimbali katika jamii na athari zake kwa maisha ya binadamu.Pia, zimekuwa zikitajwa aina mbalimbali za saratani ambazo zinawasumbua wengi katika jamii yetu.Miongoni mwake ni  ile  ya tezi dume ambayo wanataalam wanaeleza kuwa inashika nafasi ya tatu kwa kusababisha vifo vingi nchini.
Pia, wanaume wanaokunywa pombe kupita kiasi na wale wanaofanya kazi viwandani wakitajwa kuwa katika hatari zaidi ya saratani hii.Imeelezwa kuwa wanaume wanaofanya kazi katika viwanda vya rangi au wanaofanya kazi za kupaka rangi wamo hatarini zaidi.
Hata hivyo, saratani ya aina hii kwa wanaume inashika nafasi ya kwanza kwa kusababisha vifo vingi hapa nchini.Aidha,saratani ya tezi dume ni chanzo kikuu cha vifo vinavyosababishwa na saratani kwa wanaume wa umri miaka 70 na kuendelea.Hata hivyo, ni nadra kwa saratani hii kuwapata wanaume chini ya umri wa miaka 40.
Mwathirika wa saratani hiyo, na mwanzilishi wa kampeni ya kuangamiza saratani ya tezi dume ya ‘50 Plus Campaign’ Dk Emmanuel Kandusi anasema saratani hii ikitambuliwa mapema huweza kutibika.Anasema “Kutokana na ugonjwa huo kuwa hatari hapa Tanzania, ifikapo mwaka 2020 unatarajiwa kuua watu milioni 20,”

Kwa kawaida saratani ya aina hii hukua taratibu ingawa baadhi hukua kwa kasi. Seli za saratani wakati mwingine husambaa katika maeneo mengine ya mwili hasa katika mifupa na tezi za limfu.
Saratani hii inasababisha maumivu makali hasa wakati wa kukojoa.
Wengi hushindwa kushiriki tendo la ndoa, au kukosa kabisa nguvu za kiume.

Walioko hatarini kupata saratani ya tezi dume
Watu walio katika hatari kubwa ya kupata saratani ya tezi dume ni pamoja na:
•    Wanaume wenye asili ya Afrika (Weusi) ikilinganishwa na Wazungu
•    Wanaume kuanzia miaka 60 na kuendelea.
•    Wanaume wenye historia ya tatizo hili kwenye familia zao, yaani, wale ambao mmoja wa ndugu zake (kaka au mdogo wa kiume) au baba amewahi kuugua ugonjwa huu.
•    Wakulima wanaotumia aina fulani ya mbolea za kemikali.
•    Wanaofanya kazi katika viwanda vya kutengeneza matairi.
•    Wachimbaji wa madini, hususan aina ya cadmium.
•    Walaji wa chakula chenye kiasi kikubwa cha mafuta hasa ya wanyama.
Mtandao wa Wikipedia unaeleza kuwa tafiti ziliwahi kufanyika na kubaini kuwa watu waliowahi kufanya mapenzi katika umri mdogo wapo katika hatari ya kupata saratani hii.
Aidha, utafiti huo unaonyesha kuwa magonjwa ya zinaa huweza kusababisha baadhi ya kesi za saratani hii.
Dalili za saratani ya tezi dume
Katika hatua zake za awali, dalili za saratani ya tezi dume hazitofautiani  na zile za kuvimba kwa tezi dume (BPH). Dalili hizo ni pamoja na
•    Kupata shida unapoanza kukojoa
•    Kutiririka kwa mkojo baada ya kumaliza kukojoa.
•    Kukojoa mkojo wenye mtiririko dhaifu
•    Kukojoa mara kwa mara hasa nyakati za usiku
•    Kujikakamua wakati wa kukojoa na kushindwa kumaliza mkojo wote
•    Kutoa mkojo uliochanganyika na damu
•    Kutoa shahawa zilizochanganyika na damu
Vipimo vya saratani ya tezi dume
Utambuzi wa saratani ya tezi dume hujumuisha kufahamu dalili alizo nazo mgonjwa pamoja na vipimo
Digital Rectal Exam: Daktari ataingiza kidole cha shahada katika puru (rectum) ili kuhisi tezi dume kupitia ukuta wa puru. Aidha, atahisi pia sehemu zote zinazozunguka tezi dume kutambua iwapo tezi ni ngumu au kama ina uvimbe wowote.
Kwa ufupi
  • Utrasound ya Puru (Rectal Ultrasound): Kipimo hiki hufanyika iwapo daktari atahisi kuwepo kwa saratani ya tezi dume badala ya BPH. Utrasound ya puru pamoja na kuonyesha taswira ya tezi dume ilivyo, pia humwezesha daktari kuchukua kinyama (biopsy) kwenye tezi dume kwa ajili ya uchunguzi zaidi ili kutofautisha kati ya saratani na BPH.


Ni tatizo linalowasumbua watu wazima wa umri wa miaka 50 na kuendelea
Vipimo na uchunguzi
Baada ya mgonjwa kujihisi dalili zilizotajwa, daktari atamfanyia uchunguzi wa mwili kabla ya kumfanyia vipimo zaidi.
Vipimo vinaweza kutofautiana kati ya mgonjwa na mwingine, lakini baadhi ya vipimo ni pamoja na:
-Kuchunguza tezi dume kupitia njia ya haja kubwa au Digital Rectal Examination (DRE): Hiki ni kipimo cha kwanza ambacho mgonjwa hufanyiwa na daktari wake.
Ni kipimo kinachoweza kumpa daktari picha ya tatizo na kufahamu kuhusu ukubwa na hali ya tezi dume. Daktari akiwa amevaa glovu huingiza kidole chake cha shahada katika njia ya haja kubwa au puru  ya mgonjwa, kisha kuzungusha zungusha ili kufahamu kama tezi limevimba ama la, na pia hali yake kama ni gumu kuliko kawaida ama lina utando na nyama laini.
-Kipimo cha damu cha Prostate-Specific Antigen (PSA): PSA husaidia kutofautisha kati ya saratani ya tezi dume na BPH. PSA ni aina ya protini inayozalishwa na seli za tezi dume na kiwango chake huongezeka iwapo kuna saratani ya tezi dume.
-Utrasound ya Puru (Rectal Ultrasound): Kipimo hiki hufanyika iwapo daktari atahisi kuwepo kwa saratani ya tezi dume badala ya BPH. Utrasound ya puru pamoja na kuonyesha taswira ya tezi dume ilivyo, pia humwezesha daktari kuchukua kinyama (biopsy) kwenye tezi dume kwa ajili ya uchunguzi zaidi ili kutofautisha kati ya saratani na BPH.
-Kiwango cha utokaji wa mkojo (Urine Flow Study): Ni kipimo kinachotumika kufahamu kasi ya utokaji wa mkojo. Mkojo unaotoka kwa kasi na kiwango kidogo huashiria kuwepo kwa BPH.
-Kipimo cha kuchunguza kibofu cha mkojo (Cystoscopy): Kipimo hiki husaidia kuweza kufahamu ukubwa wa tezi, sehemu tezi lilipobana njia ya mkojo na kiwango cha kubana huko. Aidha, huwezesha pia kutambua hali ya kibofu cha mkojo ikoje.
Uwezo wa kufanya tendo la ndoa
Wagonjwa wengi waliofanyiwa upasuaji wa BPH huhofia kuhusu uwezo wao wa kufurahia tendo la ndoa baada ya upasuaji. Kwa kawaida, huchukua muda fulani kwa agonjwa kuweza kurejea hali ya kawaida ya kufurahia tendo hilo.

Post a Comment

POPULAR POST

 
Top