Dude amesema kuwa hakuna njia kwa sasa ya kuweza kupambana na maharamia wa kazi za wasanii zaidi kushusha bei ya filamu.
“Tumeshindwa kuwathibiti pirates, watu wanasambaza kazi, wanauza kazi kwa bei rahisi, leo hii ukienda Buguruni unapata kazi kwa elfu mbili, elfu moja mia tano, filamu ambayo wewe unaiuza dukani elfu tano wenzako wanauza elfu mbili, kwakuwa watanzania wengi ni masikini hawawezi kwenda kununua kazi elfu tatu dukani wakati anaweza kupata kazi hiyo hiyo mtaani kwa elfu moja na mia tano.
Kwahiyo hicho ndo kinachotuua sana sana, mimi kwa upande wangu kwakuwa
serikali imeshindwa kutokomeza pirates, mimi naona steps kushusha bei ni
sawa kwa sababu tunapambana na pirates, watanzania ambao wanaishi chini
ya dola moja ndo wanunuzi wa kazi zetu, sisi kazi zetu hazinunuliwi na
watu wa Masaki, watu wetu ni wa Mwananyamala, Magomeni, Gongolambo watu
ambao wanakipato cha chini, sasa mtu kama huyo kweli atumie elfu tano
yake anunue filamu? Ni wachache wanafanya hivyo ndiyo maana wanakimbilia
kununua bei ya chini, kwahiyo mimi steps naona wamechukua uwamuzi
mzuri ambao una manufaa kwetu na kwao pia,” alisema Dude.
Post a Comment