AIBU! Mwanaume
aliyetambulika kwa jina moja la Joseph amejikuta akiaibika vikali
kufuatia kudaiwa kunaswa akiwa na mwanamke mwingine ilhali yeye ni mume
wa mwanamke aitwaye Sophia, Amani limenyetishiwa.
Kwa mujibu wa mashuhuda, aibu hiyo ilimkuta Joseph, Februari 14, mwaka
huu (Siku ya Wapendanao Duniani) kwenye Kitongoji cha Nyihongo wilayani
Kahama, Shinyanga wakati wadau mbalimbali walikuwa kila mtu na wake.
Mashuhuda waliliambia Amani kwamba, Joseph ni fundi ujenzi na siku ya
tukio alinaswa kwenye nyumba inayojengwa na yeye lakini ikiwa bado
kumalizika.“Jamaa mwenye mke alishajua kuwa Jose anamlia mali zake
lakini akavumilia sana. Hakutaka kumuuliza Jose wala mke wake, yeye
alitaka amfumanie laivu mwenyewe,” alisema shuhuda.
...Wakizidi kumpa kichapo.
“Sasa siku ya tukio, Jose alionwa na mtu mmoja akiingia kwenye nyumba
inayojengwa. Yule mtu alishajua Jose anachepuka na yule mke wa jamaa,
akaenda kumwambia ndiyo wakamzukia na kumnasa,” kilisema chanzo.
Chanzo
kikaendelea kuweka wazi kuwa, baada ya Jose kunaswa alitembezewa
kichapo kizito na kupelekwa kwenye ofisi za serikali ya mtaa ambapo Jose
alipigwa faini ya shilingi laki tatu.
“Lakini
kilichotokea sasa ni kwamba, baada ya kulipa faini hiyo, mke wa Jose
naye kwa hasira aliamua kuondoka nyumbani na kwenda kwao.
Mke wa aliyefumaniwa.
“Alisema amelazimika kuondoka kwa Jose kwa sababu kitendo alichokifanya
kimemtia aibu kubwa. Kwamba haiwezekani yeye atulie nyumbani Siku ya
Wapendanao halafu mumewe akachepuke mitaani na mwanamke mwingine,”
kilisema chanzo.
Post a Comment