Kabichi
ni zao linalolimwa mahala pengi sana hapa duniani. Mboga hii imekuwa
ikiwekwa katika hadhi ya chini katika mboga, na hata watu huitumia pale
tu wanapoona hakuna jinsi ya kupata mboga ya aina nyingine. Na hivyo
utaona ikitumika katika sehemu za jumuiya kama vile shule, magerezani na
vyuoni kwani gharama yake ni ndogo hivyo huweza kuhimili hali ya
kuinunua kwa matumizi ya watu wengi.
Mboga
hii ina manufaa mengi sana mwilini lakini iwe ni mpya ya
kijani/nyekundu au hata zambarau na siyo ile iliyokaa sana sokoni hadi
kusinyaa, hiyo haina manufaa. Mboga hii ina faida zifuatazo:
kuondoa sumu mwilini
kabichi
ina Vitamin C kwa wingi kuliko hata machungwa, pi aina kampaundi za
salfa, vitu hivi huisaidia sana kusafisha damu na kuondoa sumu na
kupigana na visababishi vya saratani mwilini. Pia huimarisha ini hivyo
hulifanya lifanye kazi vizuri.
Huzuia saratani
Ulaji
wa kabichi huzuia saratani ya matiti, utumbo mpana na saratani ya
korodani (testes) kwa wanaume. Kwani ina kampaundi zinazosaidia kupigana
na visababishi vya saratani.
Huzuia uwezekano wa kupata magonjwa ya moyo
Mboga
hii huondoa lehemu katika damu kwani huleta shinikizo kubwa la damu
pale yanapojaa, na pia huweza kusababisha kiharusi na moyo kupasuka.
Hivyo kabichi husaidia kuondoa.
Ina Vitamin Muhimu kwa wingi
Kabichi ina Vitamin A, B, C, E na K kwa wingi ambazo zina faida kubwa sana mwilini kama ifuatavyo:
- Vitamin A huisaidia kuimarisha ngozi na uwezo wa kuona.
- Vitamin B huimarisha uwezo wa kutafakari na kuboresha utendaji kazi wa ubongo na kuzuia msongo wa mawazo.
- Vitamin C huimarisha kinga ya mwili na kuzuia visababishi vya saratani.
- Vitamin E hufanya ngozi yako kuwa nyororo na kuonekana kijana.
- Vitamin K huimarisha mifupa na huhusika na ugandaji wa damu pale unapoumia
Manufaa
mengine ni kama vile kulinda mwili na maambukizi ya magonjwa
mbalimbali,pia hutibu vidonda vya tumbo, kwani utafiti uliofanywa na
chuo kikuu cha tiba cha Stanford ambapo wagonjwa 13 walipona vidonda vya
tumbo kwa kunywa juisi ya kabichi mara 5 kwa siku kwa muda wa siku 7
hadi 10. Kabichi pia hutibu michubuko mbalimbali ya mwili.
Vilevile
huisaidia sana kupunguza uzito au unene kwani ina kiwango kidogo sana
cha kabohidreti na mtu anayetaka kupunguza unene na uzito anashauriwa
kula saladi ya kabichi kwa wingi.
Pia
kabichi hupunguza tatizo la kufunga choo kwani ina kambakamba
zinazosaidia kulainisha choo na Vilevile ina madini ya salfa na chuma
yanayosaidia kusafisha utumbo.
Jinsi ya kuandaa kabichi:
Kabichi
inapendekezwa sana kuliwa ikiwa mbichi kwa kuongezwa ndimu na chumvi
ili kuleta ladha nzuri kama vile kachumbari, Vilevile unaweza tu
ukaichemsha supu yake lakini isiive sana kiasi cha kuua virutubisho
vyake, inapendekezwa kuchemka kwa dakika 4 hadi 5 tu. Pia inaweza
ikakatwakatwa na kutengenezwa juisi yake kiasi cha kikombe kimoja cha
chai kinatosha. Pia inaweza kuchanganywa na mboga nyingine kama vile
mchicha au majani ya maboga.
Utunzaji:
Kumbuka
kuitunza kabichi pale unapotoka kuinunua kwa kuihifadhi katika jokofu
(friji) ili isiingie vijidudu. Vilevile kumbuka kuwa kabichi huwa ina
tabia ya kuhifadhi vijidudu pale inapotoka shambani au pia huwa na
uchafu wa mbolea au dawa za kuua vijidudu, hivyo unapaswa kuiosha sana
kwa maji safi na kuiacha ndani ya maji safi kwa muda wa nusu saa kabla
ya kuitumia ili kuua vijidudu hivi.
Angalizo:
Ulaji
wa kabichi uliopitiliza huweza kusababisha ugonjwa wa rovu (goiter).
kwahiyo watu wenye tatizo la rovu wasile kabichi kwa wingi.
Post a Comment