Wengi
tumekuwa tukitumia kama mboga au kiungo kimoja wapo katika kunogesha
mboga lakini wachache mno wanaojua faida za nyanya chungu kiafya.
Pamoja
na kufanya mboga kuwa na ladha na harufu ya aina yake, nyanya chungu
zina kazi kubwa katika mwili wa binadamu ikiwa ni pamoja na kujenga na
kuimarisha afya ya mlaji.
Nyanya
chungu ipo kwenye kundi la mbogamboga zenye virutubisho vingi ikiwemo
vitamin A, B, na C ambazo zote kwa pamoja hufanya kazi ya kuobresha afya
ya mwili kwa ujumla.
Nyanya
chungu pia husaidia kuimarisha kinga ya mwilli na kumsaidia mlaji
kuepukana na magonwja ya mara kwa mara. Hizi pia ni kinga iayoweza
kumwepusha mlaji kupata maradhi ya moyo. Kwa wagonjwa wa kisukari nyanya
chungu pia ni dawa inayoweza kusaidia katika kupunguza kiwango cha
sukari ndani ya mwili.
Vitamin
K inayopatikana ndani ya nyanya chungu inasaidia kuipa nguvu mishipa ya
damu hivyo kusaidia zoezi zima la mzunguko wa damu katika mwili wa
binadamu.
Licha ya kuwa karibu asilimia 90 ya nyanya chugu ni maji mboga hii pia inajumuisha madini ya chuma na potassium.
Post a Comment