Siku hizi anajiita King Kiba. Ni king haswaa kwakuwa nyuma yake ana mashabiki kibao walio tayari kufanya lolote kwaajili yake. Bado hajalipa jina kundi la mashabiki wake wa damu. Labda tumsaidie. The Kibaz? Wanaweza kuwa hawana jina la pamoja lakini ukweli ni huu – mashabiki wa Alikiba wana nguvu kinoma. Wachokoze uone kazi.
Huenda nguvu hii ndio sababu iliyochangia apewe shavu la kuungana na wasanii wengine wanne kutoka Kenya, Uganda, Mozambique na Nigeria kutumbuiza kwenye collabo na nyota wa Mtoni, NE-YO, kukamilisha msimu wa tatu kwa kishindo.

Kwa mashabiki wa King Kiba fursa hii ilipokelewa kwa shangwe za kutosha.Picha za behind the scenes zilizowekwa kwenye akaunti yake ya Instagram zilishambuliwa na comments kibao. Kumuona mfalme wao akiwa jukwaa moja na NE-YO kilikuwa ni kitu cha kufurahisha zaidi kukiona mwaka huu.Matarajio ni makubwa hasa kwakuwa kizuri kimewekwa mwisho. Wapenzi wa muziki wa Bongo Flava wana hamu kubwa ya kuona kile Kiba alikifanya wakati akitumbuiza na NE-YO na mastaa wengine wakiwemo Maurice Kirya, Ice Prince, Dama Do Bling na Wangechi.
Kwa niaba ya watanzania wenzangu, nina kila sababu ya kujivunia shavu hili la Kiba kuimba wimbo maalum wa kufungia msimu wa tatu wa Coke Studio Africa. Finale Episode itavuta watazamaji wengi kwenye runinga na accounti za Coke Studio Africa YouTube - fursa hiyo ni muhimu kwa Tanzania kwakuwa Kiba ataipeperusha bendera yetu. Kwa Alikiba hii ni heshima kwake kwasababu kuchaguliwa kutoka kwenye kundi kubwa la mastaa, inaonesha kuwa anakubalika.
Na pengine Alikiba hakuishia tu kufanya wimbo huo na NE-YO, kuna mengi ya ziada yaliyoendelea yatakayomsaidia zaidi. Kwakuwa Coke Studio Africa imewapa jukwaa muhimu wasanii wa Afrika, wanaojiongeza zaidi wamepata mengi na Kiba hajaachwa nyuma. Ndio maana hivi karibuni alimfuata NE-YO aliyetumbuiza jijini Kampala, Uganda kushuhudia show yake. Hakuna shaka wawili hawa wanawasiliana zaidi sasa.
Kama Alikiba hakupata ushauri muhimu wa kukuza muziki wake zaidi kutoka kwa NE-YO, basi ni lazima atakuwa amempa connection mpya za kimataifa. Na yeye mwenyewe pia anamaliza msimu kwa furaha.
Tazama tena mash up yake na Victoria Kimani, Chekecha Cheketua/Show imepigiwa kura zaidi na kuingia kwenye albamu ya mjumuisho ya Coke Studio.

Coke Studio Africa mwaka huu imetengeneza fursa nyingi kwa wasanii. Msimu huu umeliunganisha zaidi bara letu kupitia muziki. Kupitia show ya Coke Studio, kiwanda cha muziki cha Afrika kimeunganishwa katika kiwango ambacho miaka mitano iliyopita haikuwa rahisi.
Kwa utayarishaji wake wa kijanja, muziki uliotulia, wasanii wakali, bendi iliyojipanga na waandaji wenye skills za kimataifa, Coke Studio Africa ni kitu bora kabisa kuwahi kutokea kwenye muziki wa Afrika.

Post a Comment

POPULAR POST

 
Top