Haya
Wapenzi leo tutamalizia sehemu ya nne na ya mwisho ya mazoezi yapaswayo kufanywa
na wamama wajawazito.
Zoezi la
nne: Butterfly (Kipepeo)
Hili zoezi
husaidia kutayarisha misuli ya tumbo na itamsaidia mama mjamzito kutanua miguu
kwa urahisi zaidi wakati wa stage ya pili ya labor. Pia husaidia kupungua kwa
kutetemeka kwa miguu na maumivu baada ya kujifungua.
Mama
mjamzito akae chini huku akiegeza mgongo kwenye ukuta au fanicha huku
magoti yakiwa juu na miguu chini sambamba sakafuni. Mme au mtu wa karibu
na mama ataweka mikono nje
ya mapaja kama kumzuia mama wakati anajaribu kufungua miguu. Kwa hiyo
mama atafunga na kufunga miguu na mme atajaribu kumzuia. Hii itaweka resistance
kwenye misuli ya mapaja na kuyafanya yawe na nguvu zaidi. Mwanamke anapozoea
hili zoezi na kulifanya kwa urahisi basi mme anabidi kuongeza bidii katika
kumzuia ili kuongeza ugumu wa zoezi. Kumbuka haya sio mashindano kwa hiyo
haiitaji nguvu na mwanamke awe comfortable katika zoezi zima. Hili ni zoezi
gumu hivyo linaweza kufanywa mara 3 hadi 10 katika set mara moja kwa siku.
Zoezi la tano: Kegels
Hili zoezi linasaidia katika kumaintain na kutone sehemu ya
pelvic na misuli yake. Hili zoezi ni muhimu kufanywa kwa mwanamke yoyote yule.
Kuimarishwa kwa misuli hii pia kunasaidia kuongeza raha wakati wa mapenzi. Pia
husaidia kusukuma vizuri wakati wa stage ya pili ya labor. Hili zoezi pia
linasaidia misuli ya eneo hili kutokulegea baada ya kuzaa na kuendelea kuwa
tight.
Misuli hii ndio hubeba uzito wa mtoto anayekua wakati wa
ujauzito. Kutokufanya mazoezi kutasababisha misuli kulegea na kuumia kwa njia
ya uzazi wakati wa kuzaa. Hili zoezi linamsaidia mwanamke kujifunza kusukuma
mtoto vizuri wakati wa kujifungua na kuilegeza misuli ili kusaidia mtoto apite
kwa urahisi zaidi.
Wakati wa menopauase(umri ambao mwanamke anapoacha kupata siku
zake za mwezi) hormone ya estrogen inayosaidia kuipa hii misuli nguvu hupungua.
Kama misuli yako ilishalegea basi ukifika kipindi hiki unaweza kujikuta
unashindwa kuzuia kukojoa tatizo linalosababisha mkojo kutoka wakati wa kukohoa
au kupiga chafya. Hili tatizo linaweza kusaidiwa na hili zoezi hata kama misuli
yako ilishalegea.
Kama misuli hii haiko
imara basi mama anaweza kupata matatizo ya kutoweza kuzuia mkojo kutoka,
maumivu makali wakati wa kuzaa, stage ya pili ya labor kuendelea kwa muda
mrefu, kuharibika kwa misuli ya eneo hili, kusikia pressure kwenye eneo hili,
kutofurahishwa wakati wa kufanya mapenzi. Kichwa acha mtoto kukaa karibu na
kidevu wakati mtoto akiwa anashuka katika njia ya uzazi kabla ya muda wake.
Hili zoezi linafanywa kwa kushika na kuachia misuli ya
pelvis. Kama hujui hii misuli iko wapi ukienda kujisaidia haja ndogo jaribu
kuzuia mkojo na kuachia. Hii ndio misuli ya pelvic. Sasa jaribu kuendelea
kufanya hili zoezi wakati wowote kwa kubana na kuachia hii misuli huku
ukihesabu. Ongeza ugumu wa zoezi kwa kujaribu kushikilia misuli kwa dakika 2
halafu ongeza hadi dakika 3. Endelea mpaka unaweza kufanya kubana na kachia set 10 hadi 20 mara
nyingi kwa siku. Hili ni zoezi zuri kuendelea nalo muda wowote
hata baada au kabla ya kujifungua. Na hata kwa wale ambao wamemaliza kuzaa au hawajawahi kuzaa.
Mume anaweza kumpa support mkewe kwa kumkumbusha kulifanya hili zoezi. Pia
wanaume wanaweza kulifanya hili zoezi kwani wao wanahii misuli pia.
Zoezi la sita: Kurelax kwa upande na jinsi ya kulala.
Hili zoezi linasaidia kulala kwenye position ambayo ni
comfortable kwa mama na mtoto hasa wakati wa labor. Linasaidia mzunguko wa damu
na kusaidia pressure ya uzito wa mtoto kushikiliwa na kitanda badala ya mwili
wa mama. Pia kupunguza stress kwenye mwili ili uterus iweze kufanya kazi sawa
sawa wakati wa labor.
Lala upande wakati magoti yamejikunja kidogo na mguu mmoja ukae
kwa mbele. Mito ikae chini ya kichwa na maziwa. Mkono mmoja ukae kwa nyuma au juu ya kichwa.
Fanya zoezi mara mbili kwa siku, mara moja ukiwa peke yako
mara nyingine na mme au mtu wa karibu.
Mme anaweza kusaidia kwa kumkumbusha mama kufanya zoezi na kumpa
massage akikaa katika hii position hasa hasa ya mgongo. Mama anaweza pia akalala
katika position hii.
Haya ndio mazoezi yote yanayopaswa
kufanywa na mama mjamzito. Baadaye nitatoa ratibu maalumu ya kufanya
haya mazoezi ili ujue jinsi ya kuyapangalia katika muda wako wa kila
siku.
Post a Comment