BAADA YA ZITTO KUVULIWA UONGOZI CHADEMA..MAKAMU MWENYEKITI WA CHADEMA
BARA NAE AJIUZULU LEO, SOMA BARUA YAKE YA KUJIUZULU HAPA!!
Salaam,
Napenda kuwasilisha kwako taarifa ya kujiuzulu nafasi ya Makamu
Mwenyekiti Bara kuanzia Leo Ijumaa 22 Novemba 2013 kwa kuchoshwa na
Unafiki unaoendelea ndani ya Chama. Napenda ifahamike pia kwangu maslahi
ya Wapiga kura, Wakaazi na wananchi wa Mpanda Mjini na Wilaya ya Mpanda
ni muhimu katika kuwatumikia, hivyo basi sipo tayari kuchaguliwa
marafiki.
Kwa kipindi kirefu
zimekuwepo shutma dhidi yangu na kutiliwa mashaka mahusiano yangu na Mhe
Pinda Waziri Mkuu pamoja na kulijadili katika vikao kadha Mpanda na Dar
es Salaam bado yapo mashaka kwa nini alipita bila kupingwa hayo yalikua
maamuzi ya Wanampanda kwenu imekua ni tatizo lakin hamsemi kwa nini
Majimbo mengine 16 nchini yalipita bila kupingwa mlikua wapi na nani
alaaumiwe huu ni Unafiki wa kupindukia.
Aidha mmechukizwa
sana kwa nini nilihoji kauli ya Muasisi wa Chama Mhe Mtei kutuchagulia
viongozi naomba ifahamike wazi kwamba huu ni mtazamo wangu na utabakia
hivyo siku zote kwa chama cha demokrasia kutoruhusu uongozi wa kiimla
kwa kukidhi matakwa ya Waasisi ambao huvigeuza vyama kuwa Mali binafsi
Kwa kusema ukweli na kusimamia ukweli daima itabakia kuwa lengo langu
katika maisha yangu siku zote hata kama itanigharimu maisha yangu.
Nawasilisha.
Said A Arfi (mb)
BAADA YA ZITTO KUVULIWA UONGOZI CHADEMA..MAKAMU MWENYEKITI WA CHADEMA BARA NAE AJIUZULU LEO, SOMA BARUA YAKE YA KUJIUZULU HAPA!!
Salaam,
Napenda kuwasilisha kwako taarifa ya kujiuzulu nafasi ya Makamu Mwenyekiti Bara kuanzia Leo Ijumaa 22 Novemba 2013 kwa kuchoshwa na Unafiki unaoendelea ndani ya Chama. Napenda ifahamike pia kwangu maslahi ya Wapiga kura, Wakaazi na wananchi wa Mpanda Mjini na Wilaya ya Mpanda ni muhimu katika kuwatumikia, hivyo basi sipo tayari kuchaguliwa marafiki.
Kwa kipindi kirefu zimekuwepo shutma dhidi yangu na kutiliwa mashaka mahusiano yangu na Mhe Pinda Waziri Mkuu pamoja na kulijadili katika vikao kadha Mpanda na Dar es Salaam bado yapo mashaka kwa nini alipita bila kupingwa hayo yalikua maamuzi ya Wanampanda kwenu imekua ni tatizo lakin hamsemi kwa nini Majimbo mengine 16 nchini yalipita bila kupingwa mlikua wapi na nani alaaumiwe huu ni Unafiki wa kupindukia.
Aidha mmechukizwa sana kwa nini nilihoji kauli ya Muasisi wa Chama Mhe Mtei kutuchagulia viongozi naomba ifahamike wazi kwamba huu ni mtazamo wangu na utabakia hivyo siku zote kwa chama cha demokrasia kutoruhusu uongozi wa kiimla kwa kukidhi matakwa ya Waasisi ambao huvigeuza vyama kuwa Mali binafsi
Kwa kusema ukweli na kusimamia ukweli daima itabakia kuwa lengo langu katika maisha yangu siku zote hata kama itanigharimu maisha yangu.
Nawasilisha.
Said A Arfi (mb)
Post a Comment