Kwa miezi sita ya
kwanza katika maisha ya mtoto chakula pekee ambacho wataalamu wa afya
wanashauri apewe ni maziwa ya mama tu. Kunyonyesha ndio njia ya kwanza kabisa
kumpa mtoto chakula. Unapoanza kumpa mtoto vitu vingine kama maziwa ya kopo
wakati ana miezi michache utoaji wako wa maziwa unaathirika maana jinsi mtoto
anavyonyonya ndivyo jinsi maziwa yanavyotengenezwa ndio maana watu wengi
wanavyoanza kazi na kumuacha mtoto nyumbani maziwa yao yanaanza kupungua. Faida
za kunyonyesha maziwa ya mama ni pamoja na:
Maziwa ya mama yana
virutubisho vingi vya asili ambavyo ni muhimu sana katika ukuaji na kinga kwa
mtoto. Humlinda na magonjwa mengi ya utoto pamoja na ‘allergies’ mbalimbali.
·
Hukuwezesha kuwa na ukaribu na mtoto
wako.
·
Hukupunguzia uwezekano wa kupata kansa
ya matiti.
·
Ni bure na unaweza kumpatia maziwa
wakati wowote bila usumbufu.
Wakati
gani Uanze Vyakula Vingine
Mtoto wako akifikisha
miezi 6 unaweza kuanza kumpatia vyakula vingine kidogo kidogo (Kuna ambao
kutokana na sababu Fulani daktari huwashauri kuanza mtoto akiwa na miezi 4
hivyo ni vyema ukiwasiliana na daktari
wako kwanza). Mtoto akianza kupewa vyakula nje ya maziwa mapema kabla ya miezi
4 ni hatari kwa afya yake maana mfumo wake wa kusaga chakula unakuwa bado
haujawa tayari. Unapoanza kumpa vyakula vingine hauachi kumnyonyesha,
unyonyeshaji unaendelea hadi miaka miwili na nusu.
Dalili
kuwa mtoto wako yupo tayari kuanza vyakula vingine ni:
·
Amefikisha miezi 6
·
Anaweza kushikilia kichwa juu ( shingo
imekaza)
·
Anaweza kukaa kwa kuwekewa kitu ( mfano
kiti chenye mkanda)
·
Unapompa chakula na kijiko anafungua
mdomo kutaka kupokea au anageuza uso kwa kukataa
·
Akipokea chakula anakiweka mdomoni na
kujaribu kumeza na sio kukisukuma nje na kuacha mdomo wazi.
Hakikisha mtoto wako
yupo tayari kabla hujaanza kumpa chakula na usimlazimishe sana anapoanza maana
anaweza kuchukia chakula, inawezekana hapendi chakula ulichompa jaribu
kubadilisha uone anapenda nini. Kila mtoto ni tofauti na mwingine hivyo
usimlinganishe mtoto wako na mwingine la muhimu ni kuhakikisha kuwa anauzito
kulingana na umri wake na anaongezeka kwa kupanda chati.
Mnapokuwa mnakula
mezani mtoto naye awe hapo ili kumpa hamu ya kula na sio kila wakati akila
anakuwa peke yake. Mpe chakula akiwa na furaha na pia akiwa na njaa ili aweze
kufurahia chakula chake. Kabla ya kubadilisha aina ya chakula mpe kwa siku 3-4
mfululizo ili aweze kukizoea na kama kitamletea madhara ujue hasa ni chakula
gani. Usimchanganyie vyakula maana hutajua anapenda nini na kuchukia nini na
pia kama kuna kitu kitamdhuru ukichanganya hautagundua kwa urahisi.
Miezi
6-9
Endelea kunyonyesha na
anza kumpa vyakula vyenye madini ya chuma. Mtoto alishwe kwa ratiba
inayoeleweka kila siku na katika ratiba hiyo hakikisha angalau mara moja kwa
siku muda wake wa kula unakuwa sawa na muda wa familia yote ili muweze kula
pamoja. Vyakula vyake viwe vimepondwapondwa kabisa ikiwezekana tumia blender na
hakikisha anapata mlo kamili yani matunda, mbogamboga, mbegu, nafaka, nyama na
samaki. Inashauriwa kutokuchanganya aina tofauti za nafaka kwenye unga mmoja
unapomtengenezea uji, uwe na unga wa mahindi, ulezi,mchele n.k tofauti tofauti.
Pika aina moja ya uji kwa wakati unaweza kufanya kwa wiki au vyovyote
utakavyopenda.
Unapompa mboga au
matunda anza na tunda moja moja kwa wakati. Osha vizuri matunda yako na
katakata vizuri na kuponda ponda kisha mpe kiasi kidogo kwa wakati na kikibaki
usikiweke, mtengenezee kile atakachokula tu. Matunda kama papai, parachichi na
embe ni mazuri kwa kuanzia. Chemsha maharage, njegere au mboga za majani na
kumpa supu kidogo kidogo, usiweke chumvi nyingi kidogo sana inatosha. Usimpe juisi
za madukani, hakikisha unamtengenezea juisi wewe mwenyewe na usichanganye
matunda mbalimbali kwenye juisi moja, na usiweke sukari kabisa.
Miezi
9-12
Katika umri huu mtoto
anakuwa tayari amezoea ladha tofauti tofauti za vyakula mbalimbali nje ya
maziwa. Anauwezo wa kukaa na kushikilia kitu kwa mikono yake na kuweka mdomoni
hivyo anza kumpa matunda laini mkononi aanze kujifunza kula mwenyewe. Hakikisha
vipande sio vidogo sana anavyoweza kumeza ili kuepuka hatari ya kukabwa. Kwa
sababu pia atakuwa ameanza kuota meno atakuwa anapenda sana kutafuna tafuna.
Katika umri huu pia unaweza kuanza kumpa kiini cha yai, ute wa yai hadi afike
umri wa mwaka mmoja. Endelea kumnyonyesha ila kwa sasa anakula kwanza kisha
ndio ananyonya maana akinyonya sana anaweza akakataa chakula. Usimpe chakula
kimoja mfululizo kwa muda mrefu maana atakinai na kuanza kukataa chakula, mpe
vyakula tofauti tofauti ili aendelee kupenda chakula.
Jinsi
ya Kutengeneza Chakula cha Mtoto
Ni rahisi sana
kutengeneza chakula cha mtoto nyumbani kwako. Osha mikono yako vizuri kabla ya
kuandaa chakula na hakikisha unatumia vyombo visafi.
Matunda
na mboga mboga: osha mboga zako vizuri kwa maji safi (
ya uvugu vugu) na kisha katakata na kubandika jikoni kwa chumvi kidogo sana
bila mafuta. Ikichemka isage kwenye blender au ponda ponda iwe laini kabisa
kisha mpe mtoto. Matunda osha pia kwa maji ya uvugu vugu, toa ganda la nje na
kata vipande vikubwa kama unataka ale kwa mikono yake mwenyewe au ponda ponda
na upe kwa kijiko.
Nyama
na Samaki: Chemsha vipande vya nyama na maji kidogo na iive
kwa moto wa kiasi hadi ilainike kabisa kisha isage kwenye mashine (food
processor) na umpe na ile supu. Samaki vile vile ila samaki hakuna haja ya
kuisaga maana ikiiva inalainika sana na ni rahisi kwa mtoto kula bila taabu
(Kuwa makini sana na mifupa!).
Mbegu:
Hapa nazungumzia maharage, kunde, choroko, njegere n.k Pika hadi ziive kabisa
na kulainika kisha pondaponda na kumpa mtoto. Pia viazi na ndizi vinafaa sana
kwa watoto, unaweza ukachanganya na supu ya samaki / nyama au na maziwa.
Nafaka:
Usichanganye nafaka tofauti tofauti kwa ajili ya uji wa mtoto, inashauriwa kuwa
na unga tofauti kwa kila nafaka. Unapopika uji unaweza kuweka karaga
zilizosagwa ili kuongeza mafuta na vitamin kwenye lishe ya mtoto.
Usalama
katika Kula
·
Hakikisha haumuachi mtoto mdogo na
chakula au kinywaji bila uangalizi hata kama ni maziwa ya chupa asije
akapaliwa. Usimpe mtoto chakula au maziwa akiwa amelala, analia au anacheka.
·
Usimpe chakula ambacho kinaweza kumkaba
au kumpalia kama karanga, maindi, zabibu n.k
·
Kabla ya kumpa mtoto chakula hakikisha
umekiangalia joto lake usije ukamuunguza mdomo.
·
Usafi wa mtayarishaji, mlishaji na
mlishwaji ni muhimu san asana.
Post a Comment