Upungufu
wa damu (anaemia) hutafsiriwa kama kupungua kwa kiwango cha hemoglobin
katika damu damu chini ya kiwango kinachokubalika kiafya. Kiwango cha
kawaida cha haemoglobin (Hb) katika mwili wa binadamu ni kati ya gramu
12 mpaka 14 kwa kila mililita ya damu. Hata hivyo shirika la afya
duniani (WHO) linatambua kiwango cha mpaka 11gm/mililita kuwa cha
kawaida kwa mama mjamzito. Hivyo basi mjamzito mwenye kiwango chochote
cha haemoglobin chini ya 11 gm/mililita hutafsiriwa kuwa na upungufu wa
damu. Hata hivyo nchi nyingi hasa zinazoendelea hutambua kiwango cha
mpaka gramu 10 kwa mililita kuwa ni upungufu wa damu kwa mjamzito.
Kwa
mjamzito anayehudhuria kliniki kwa mara ya kwanza, upungufu wa damu
kipindi cha ujauzito humaanisha kiwango cha hemoglobin chini ya <11.0
g/dL, na mimba inapofikisha wiki 28 upungufu wa damu hutambuliwa iwapo
hemoglobin itashuka na kuwa chini ya 10.5 g/dL.
Kwa
kuzingatia hilo, mama mjamzito hushauriwa kupima wingi wa damu siku
anapohudhuria kliniki kwa mara ya kwanza na pindi mimba inapofikisha
wiki 28.
Viwango vya Anaemina.
Upungufu
wa damu unaweza kugawanywa katika viwango vikuu vinne, yaani upungufu
wa damu wa kawaida (mild anaemia) ambao ni kati ya 9-11 gm/ml, upungufu
wa damu wa kati (moderate anaemia) ambao ni kati ya 7-9 gm/ml, upungufu
wa damu mkali (severe anaemia) ambao ni kati ya 4-7 gm/ml na upungufu wa
damu mkali zaidi (very severe anaemia) ambao ni chini ya 4gm/ml.
Mzunguko wa madini ya chuma mwilini.
Kwa
kawaida mwili wa mwanamke huifadhi gramu 3.5 mpaka 4.5 za madini ya
chuma. Asilimia 75 huifadhiwa kama hemoglobin katika chembe damu
nyekundu, asilimia 20 kama ferritin katika mifupa na asilimia 5
inayobaki huifadhiwa katika misuli na vimeng’enyo vingine vya mwili.
Wanawake
wasio wajawazito hupoteza karibu gramu 1 za madini ya chuma kutoka
katika seli za mwili zinazokufa kila siku na gramu 1 zaidi kila siku
wanayokuwa kwenye hedhi.
Ukubwa wa tatizo.
Upungufu
wa damu kipindi cha ujauzito ni tatizo linalowakumba kina mama
wajawazito wengi sana, siyo tu Tanzania bali nchi nyingi zinazoendelea.
Inakisikiwa kuwa karibu theluthi moja ya wajawazito katika miezi mitatu
ya mwisho ya ujauzito hukumbwa na tatizo hili.
Kwa
mujibu wa WHO, inakadiriwa kuwa karibu asilimia 56 ya wajawazito huko
kusini mashariki ya Asia hukumbwa na tatizo hili. Kwa hapa Tanzania,
hakuna takwimu sahihi kuhusu tatizo hili. Sehemu nyingine duniani,
inakadiriwa kuwa karibu asilimia 4-16 ya vifo vinavyotokana na ujauzito
husababishwa na upungufu wa damu. Aidha upungufu wa damu wakati wa
ujauzito huongeza uwezekano wa madhara kwa mtoto ikiwemo kifo.
Chanzo cha upungufu wa damu wakati wa ujauzito.
Kipindi
cha ujauzito huambatana na mabadiliko mbalimbali ya mwili. Moja ya
mabadiliko hayo ni ongezeko la maji (plasma volume) katika mzunguko wa
damu. Katika hali hii, pamoja na kwamba kiasi cha damu huonekana
kuongezeka, kiwango cha hemoglobini hupungua mpaka kufikia 11.5mg/dl.
Karibu
asilimia 85 ya anaemia wakati wa ujauzito husababishwa na upungufu wa
madini ya chuma mwilini. Upungufu wa madini ya chuma unaweza
kusababishwa na kula chakula chenye kiasi kidogo cha madini haya au
mwili wa mjamzito kushindwa kutunza madini ya chuma ya kutosha kutokana
na ama mimba zilizopita au kupoteza kiasi kingi wakati wa hedhi kabla ya
kushika mimba.
Vyanzo vingine ni pamoja na
Upungufu wa folic acid
Ugonjwa wa sickle cell
Lishe duni kabla na wakati wa ujauzito
Kupoteza damu kwa sababu ya kuumia au kuwa na minyoo (hookworms)
Ugonjwa wa malaria wakati wa ujauzito
Ugonjwa wa chembe damu nyekundu ujulikanao kama beta thalassaemia. Ugonjwa huu huwapata zaidi watu wanaoishi Asia ya kusini, Ulaya ya kusini na Afrika.
Upungufu wa vitamin B12
Ugonjwa sugu wa kuvunjika chembe damu nyekundu (chronic haemolysis) kama vile ugonjwa kurithi wa chembe damu nyekundu (hereditary spherocytosis)
Ugonjwa wa kupoteza hemoglobin kupitia mkojo (paroxysmal nocturnal hemoglobinuria)
Saratani ya damu (leukemia)
Matatizo ya kupoteza damu kwenye njia ya chakula (gastrointestinal bleeding)
Matatizo katika utumbo hasa wakati wa ujauzito.
Upungufu wa folic acid
Ugonjwa wa sickle cell
Lishe duni kabla na wakati wa ujauzito
Kupoteza damu kwa sababu ya kuumia au kuwa na minyoo (hookworms)
Ugonjwa wa malaria wakati wa ujauzito
Ugonjwa wa chembe damu nyekundu ujulikanao kama beta thalassaemia. Ugonjwa huu huwapata zaidi watu wanaoishi Asia ya kusini, Ulaya ya kusini na Afrika.
Upungufu wa vitamin B12
Ugonjwa sugu wa kuvunjika chembe damu nyekundu (chronic haemolysis) kama vile ugonjwa kurithi wa chembe damu nyekundu (hereditary spherocytosis)
Ugonjwa wa kupoteza hemoglobin kupitia mkojo (paroxysmal nocturnal hemoglobinuria)
Saratani ya damu (leukemia)
Matatizo ya kupoteza damu kwenye njia ya chakula (gastrointestinal bleeding)
Matatizo katika utumbo hasa wakati wa ujauzito.
Vihatarishi vya tatizo.
.Masuala
ya kijamii kama vile umri wa mjamzito, kiwango chake cha elimu na
uelewa kuhusu afya yake, kama ana mwenza wa kumsaidia kiuchumi, makazi
anayoishi vinaweza kuchangia mjamzito kupata upungufu wa damu
.Vihatarishi
vingine ni vile vinavyohusu masuala ya uzazi kama vile idadi ya mimba
zilizotanguli (waliowahi kuzaa wana hatari ya kupata anaemia kuliko
wanaopata mimba kwa mara ya kwanza), kuwa na mimba ya mapacha na kuwa na
historia ya kuzaa mtoto njiti
.Vihatarishi
vingine vinahusu tabia za mjamzito kama vile uvutaji sigara, unywaji wa
pombe na kutohudhuria kliniki wakati wa ujauzito
.Pia kuwa na magonjwa kama vile kisukari, magonjwa ya figo, pamoja na shinikizo sugu la damu
Madhara na upungufu wa damu kwa mama na mtoto.
Sehemu
nyingine duniani, inakadiriwa kuwa karibu asilimia 4-16 ya vifo
vinavyotokana na ujauzito husababishwa na upungufu wa damu. Aidha
upungufu wa damu wakati wa ujauzito huongeza uwezekano wa madhara kwa
mama na mtoto ikiwemo kifo. Madhara haya ni pamoja na
.Madhara
kwa mama kipindi cha ujauzito: kukonda au kuongezeka uzito kwa kiasi
kidogo sana, kuhisi uchungu kabla ya muda, kondo la nyuma kutunga
pasipostahili, shinikizo la damu wakati wa ujauzito, na chupa kupasuka
kabla ya wakati.
.Madhara
kwa mama wakati wa kujifungua: kupatwa na uchungu usioeleweka na usio
wa kawaida, mtoto kuvuja damu ndani kwa ndani, kupatwa na shock, hatari
ya ganzi (anesthesia risk) kwa anayefanyiwa upasuaji, na moyo kushindwa
kufanya kazi.
.Madhara
kwa mama baada ya kujifungua: maambukizi baada ya kujifungua, kizazi
kushindwa kurudi katika hali ya kawaida au damu kuganda kwenye mishipa.
.Madhara
kwa mimba na mtoto atakayezaliwa: Madhara ni pamoja na mtoto kuzaliwa
njiti, mtoto kuzaliwa na uzito mdogo, mtoto kuwa na score ndogo (poor
Apgar score), mtoto kuzaliwa akiwa amechoka (fetal distress), na
upungufu wa damu kwa mtoto
Watoto
wanaozaliwa wakiwa na upungufu wa damu hukua kwa tabu, huwa na
maendeleo duni ya kiakili na kimatendo (poorer intellectual
developmental milestones), uwezekano mkubwa wa kuwa na kasoro mwilini na
hata kifo. Kasoro hizo ni pamoja na matatizo ya magonjwa ya moyo ya
kuzaliwa nayo (congenital heart diseases)
Dalili.
Mjamzito
mwenye upungufu wa damu wa kawaida mara nyingi anaweza asioneshe dalili
zozote. Hata hivyo iwapo upungufu ni mkubwa, dalili za awali ni pamoja
na uchovu wa mara kwa mara na kupumua kwa shida, kukosa hamu ya kula,
mapigo ya moyo kwenda kasi, na kuchafuka kwa tumbo.
Wakati
wa uchunguzi mjamzito anaweza kuonekana mweupe kuliko kawaida hasa
sehemu za viganjani, kucha za vidoleni, ulimi, au macho. Anaweza pia
kuwa na dalili za kuvimba miguu.
Dalili nyingine ni kama zilivyoelezwa katika makala iliyopita ya upungufu wa damu.
Vipimo vya uchunguzi.
Uchunguzi
wa upungufu wa damu hufanywa kuwa kupima kiasi cha haemoglobin pamoja
kufanya kipimo kingine cha damu kijulikanacho kama peripheral smear.
Vipimo
vingine vya maabara ni pamoja na kipimo cha kufahamu uwezo wa kuhifadhi
madini ya chuma yaani total iron binding capacity (TIBC), kiasi cha
feritin katika damu, kiasi cha folic acid. Katika mazingira mengine
kipimo cha kuchukua sehemu ya supu ya mifupa na kuichunguza maabara
yaani bone marrow biopsy kinaweza kufanywa. Hata hivyo hivi si vipimo
vinavyofanywa mara kwa mara.
Matibabu.
Mama
mjamzito huitaji miligramu 2 mpaka 4.8 za madini ya chuma kila siku.
Ili aweze kupata kiasi hiki, inampasa kula kati ya miligramu 20 mpaka 48
za madini ya chuma. Kwa jamii ambayo upatikanaji wa vyakula vyenye
madini hayo ni wa shida, suala hili linaweza kuwa gumu sana
kutekelezeka, ndiyo maana Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imeweka
mpango maalum wa kuwapa wajawazito wanaohudhuria kliniki madini ya chuma
na folic acid ili kufidia pengo hilo.
Vidonge
vya madini ya chuma ni salama, nafuu na njia makini ya kuongeza na
kurekebisha upungufu wa damu mwilini. Kwa wajawazito ambao hawawezi
kunywa, kwa sababu yeyote ile, njia ya sindano inaweza pia kutumika.
Wajawazito
wanashauriwa kutumia miligramu 60 za madini ya chuma (ferrous sulphate)
na 500mg za folic acid kila siku, ambapo utaratibu huu huendelea kwa
miezi mitatu mpaka sita ili kuongeza hifadhi ya madini ya chuma mwilini,
hata kama kiwango kinachotakiwa kitakuwa kimefikiwa.
Utumiaji wa vidonge vya madini ya chuma na baadhi ya chakula.
Vikiliwa
wakati mjamzito amekunywa vidonge vya madini ya chuma vinaweza
kupunguza unyonyaji wake katika utumbo. Kwa upande mwingine baadhi ya
vyakula vyenye vitamini C kama vile matunda ya jamii ya machungwa
huongeza uwezo wa utumbo kunyonya madini ya chuma mwilini.
Vyakula vya kuongeza damu.
Pamoja
na mkakati huo, wajawazito hushauriwa pia kula vyakula vyenye madini ya
chuma kwa wingi kama vile nyama, maini, mayai, samaki, mimea jamii ya
kunde, maharage makavu, mboga za majani, matembele, na mikate
iliyoongezwa madini ya chuma.
Matibabu ya upungufu wa damu mkali kwa wajawazito walio katika wiki za mwisho(baada ya wiki ya 32)
Wagonjwa
wa kundi hili hutibiwa hospitali. Wengi wanaweza pia kuwa na dalili za
matatizo ya moyo, hivyo wanapaswa kulazwa na kupumzika kitandani, na
wakati fulani kuongezewa hewa ya oksijeni. Pamoja na kutibiwa matatizo
ya moyo, huongezewa pia damu (packed red cells) kwa vile vidonge vya
madini ya chuma havitafaa kurekebisha tatizo hili kwa haraka kabla ya
muda wa kujifungua kufika.
Matibabu ya maradhi mengine.
kwa
mazingira yetu, magonjwa kama malaria na minyoo huchangia kwa kiasi
kikubwa kutokea kwa upungufu wa damu kwa wajawazito, hivyo basi magonjwa
haya hayana budi kutibiwa kikamilifu ili yasilete madhara kwa mjamzito.
Wajawazito wanaoishi maeneo yenye malaria kwa wingi hupewa dawa za SP
kwa ajili ya kuwalinda wasipatwe na ugonjwa huu. Pia dawa za minyoo za
Albendazole au mebendazole hutolewa kwa wajawazito baada ya miezi mitatu
ya mwanzo ili kuua minyoo. Ili kuzuia kujiridia kwa minyoo, wajawazito
pia hushauriwa kuvaa viatu/kandambili kila wakati, na kuhakikisha miili
na mazingira yao yapo safi.
Post a Comment