Miaka ya zamani wanawake waliokuwa na kifafa walikuwa wana shauriwa kutopata mimba kutokana na kifafa. Lakini mambo siku hizi yamebadilika, thanks to prenatal care  (dawa wanazopewa akina mama wajawazito ili kusaidia kumwandaa mtoto na mama vyema wakati waujauzito).

Hivyo basi kama una kifafa lakini unataka kubeba mimba, ni mambo gani muhimu ya kiafya unahitaji kujua ili kuilea mimba yako vyema. 

JE KIFAFA KINA MFANYA MAMA APATE TABU/UGUMU WA KUSHIKA MIMBA AMA KUJIFUNGUA?
Kila mwanamke anamaumbile tofauti hivyobasi, katika wanawake wenye ugonjwa wa kifafa wako ambao hupata siku zao za mwezi zikiwa zimepishana pishana (irregular menstrual cycles) na matatizo mengine ya kizazi/ukeni mfano; uvimbe wa ovari  (polycystic ovarian syndrome) kitendo ambacho kinaweza kumpa mama mjamzito matatizo ya ugumu wa kushika mimba. 
Pia kama mtu anatumia madawa ya kifafa hii inaweza kusababisha kuingiliana na mambo ya fertility hence kusababisha kutokuweza kushika mimba kiurahisi. However, having said that haimaanishi mwanamke mwenye kifafa hawezi kupata mimba kirahisi. Kunauwezekanao mkubwa tuu wakushika mimba na kuzaa mtoto mwenye afya njema kabisa. 


Hivyobasi, mwanamke mwenye KIFAFA ana affectiwa vipi akishika mimba? mara nyingi huexperience yafuatayo;
Kujisikia vibaya/na kuwa na kichefuchefu kikubwa sana asubuhi
Kupungukiwa kwa damu
Kutokwa na damu katika uke wakati na baada ya kujifungua
Maumivu ya tumbo
Plasenta kuanza tofauti na ukuta wa mimba (uterus) kabla ya mtoto kuzaliwa.
High blood pressure na uwingi wa protein kwenye mkojo baada ya wiki 20 za ujauzito (hii inaitwa preeclampsia)
Mtoto kuzaliwa mapema kabla ya tarehe zake
Uzito mdogo wa kichanga
Kupata matatizo wakati wa kujifungua
Mtoto kuwa na matatizo yaliyosababishwa wakati wa kuzaliwa
cleft palate
Hali ya Afya ya mzazi mwenye KIFAFA baada ya kujifungua
Kila mwanamke mwenye ugonjwa wa kifafa ni tofauti. Wengine wakishajifungua mshtuko wa moyo (seizures) hubakia kama zilivyokuwa toka mwanzo kabla ya kuwa mjamzito na wengine mshtuko hupungua kwa kiasi kikubwa. Kama kifafa hakikuwa controlled vizuri though toka mwanzo hii ni ikimaanisha kwamba kabla ya mimba na wakati wa mimba, huweza kuongeza ukubwa wa mshtuko katika moyo (seizures).

MADAWA!
DAWA zozote zinazomezwa na mama mwenye kifafa anapokuwa mjamzito huweza kumuaffect mtoto akiwa tumboni. Mfano; mtoto anaweza kutoka na mdomo kupasuka kwa juu (cleft palate), matatizo katika uti wa mgongo, matatizo yamifupa kutokujiunda vizuri, matatizo ya moyo n.k. 

CHAKUZINGATIA ni kutokunywa dawa za kucontrol seizures zenye dosage nyingi wakati mama yuko mjamzito. Kwamaana kutokucontrol seizures inaweza kumnyima mtoto oxygen therefore kusababisha matatizo as well. Hata hivyo seizures zinaweza pia kuongeza risk ya miscarriage. 

Having said the above, haimaanishi mama mwenye kifafa na ambaye mjamzito ndo aache kunywa dawa kwasababu zitamletea matatizo kwake na mtoto, hapana. MARANYINGI dactari wa mama mjamzito aliye na kifafa atatoa ushauri wa dawa gani za kunywa na dozi kiasi gani. 

Pia kitu kingine, kuna chances kubwa kwamba mtoto akiwa anakuwa mkubwa na yeye anaweza kudevelop seizures za hapa na pale. 

CHAMSINGI kwa mama aliyemjamzito na mweye kifafa, ni muhimu;
Kula chakula bora wakati wa ujauzito
Kunywa dawa kama zilivyo agizwa na doctor za kuweza kucontrol seizures wakati wa ujauzito
Kula vitamins
Kuhakikisha stress kwenye mwili iko chini
Kupumzika kwa kutosha (kulala)
Kutovuta sigara ama kukaa mahali watu wanavuta sigara ili kuepuka kuuvuta moshi wa sigara
Kutokunywa pombe
Kupunguza caffeine kwenye chakula ama vinywaji
Kuzuia kuwa karibu na vitu vyenye chemikali i.e. kama rangi, dawa za kuuwa wadudu etc



Post a Comment

POPULAR POST

 
Top