Tatizo la kutokwa na chunusi ni ugonjwa wa ngozi ambao hushambulia sehemu za usoni  na kuharibu sura ya mwanadamu hasa wanawake.
Ugonjwa huu umekuwa ukiwachukiza baadhi ya wanawake na wanaume kutokana na kuharibika kwa uso wao na matokeo yake kujikuta wakienda kununua vipodozi  vyenye kemikali kali ambazo ni hatari kwa afya ya ngozi zao.
Vipodozi hivyo ni hatari kwani vingine huweza kuchubua na kusababisha ngozi kukosa kinga,hivyo kuleta madhara  makubwa mwilini.
Chunusi huwatoka na kuwasumbua watu wengi hasa vijana wenye umri wa kubalehe  lakini pia hushambulia hata watu wazima.
Ukitokwa na chunusi maana yake una mchanganyiko wa magonjwa tofauti ya ngozi sehemu za usoni kwani vipele vidogo vinavyotoka husababisha maumivu na muwasho kwa muathirika.
Vipele hivyo baadaye hutunga usaha na kuwa chunusi ngumu.
Kitaalamu  ili mtu awe na chunusi kuna vijidudu hushambulia vitezi vya ngozi ya uso vijulikanavyo kwa jina la Pilosebaceous na Sebaceous gland.
 Tezi hizi hutoa mafuta mengi usoni na yakizidi huwa chakula cha vijidudu (bacteria)wanaokaa kwenye ngozi na kusababisha uingiaji wa vidudu hivyo kwenye hizo tezi  na kusababisha chunusi.
Chunusi hutokea baada ya tezi za Pilosebaceous kuziba (obstruction), huzibwa na mgando wa mafuta ya usoni na kusababisha wadudu kuingia kwenye tezi za usoni ambapo wadudu hao hushambulia ngozi ya usoni.

MADHARA YA CHUNUSI

Mdudu anayesumbua hujulikana kwa jina la Propionibacterium acnes, madhara ya mdudu huyo hutegemea na jinsi alivyoivamia ngozi kwani akiingia ndani zaidi  husababisha uvimbe wenye maumivu.
Madhara mengine ni kutoka vipele vidogovidogo ambavyo vinaweza kuwa haviumi lakini kuharibu sura ya aliyenavyo.
Kwa kawaida chunusi hutokea kwa mtu ambaye amefikia hatua ya balehe au wakati mwanamke akiwa kwenye siku zake za hedhi au akiwa mjamzito.
Hii ni kwa sababu wakati huo homoni ya Androgen huzalisha mafuta ya ngozi ya usoni (sebum) kwa wingi.
Vitu vingine vinavyochangia chunusi ni uchafu kwa kutokuosha vizuri uso, kutumia sabuni kali na kula chokuleti kwa wingi .
Wakati wa kiangazi chunusi hupungua kwa sababu mwanga wa jua huyeyusha mafuta ya usoni na kusababisha uso ung’ae.

Post a Comment

POPULAR POST

 
Top