Kitunguu
swaumu ni jamii ya vitunguu ambayo kwa kitaalamu huitwa Allium sativum.
Jamii hii ilianza kutumika katika mabara mbalimbali duniani hususani
Asia, Afrika na Ulaya takribani miaka 6000 iliyopita. Matumizi makuu
nyakati hizo yakiwa viungo katika mboga na tiba.
Kitunguu
swaumu kimetajwa kwenye vitabu mbalimbali vya dini vikielezea faida
zake katika kutibu maradhi mbalimbali yasababishwayo na bakteria,
matatizo katika mapafu, matatizo katika mfumo wa umen'genyaji chakula,
na matatizo ya kuishiwa nguvu.
Historia
inaonesha kuwa, vitunguu swaumu vilianza kutumika China mwaka 510 K.K
na pia vilitumiwa na wanajeshi wa Ugiriki na Roma. Aidha wasafiri wa
vyombo vya baharini na vijijini pamoja na wakulima barani Afrika
walivitumia sana.
Mwaka
1858, mtafiti na mwanasayansi wa nyakati hizo, Louis Pasteur aligundua
uwezo wa kitunguu swaumu katika kuua vimelea mbalimbali vinavyosababisha
magonjwa, na hivyo vikaanza
kutumika
kama dawa ya kusafishia vidonda na kuzuia kidonda ndugu hasa zama za
vita ya kwanza na pili ya dunia. Isitoshe, mpaka sasa zipo dawa kadhaa
zilizotengenewa kwa kutumia jamii hii ya
vitunguu
swaumu ikiwemo dawa ya kusafisha mdomo (mouth wash) ingawa watumaiji
wake wengi huilalamikia dawa hiyo kwa sababu ya harufu mbaya ya dawa
hiyo inayowasababishia kunuka kwa mdomo.
Faida za vitunguu swaumu
Katika
tafiti mbalimbali vitunguu swaumu vimeonekana kuwa na uwezo wa kutibu
maambukizi ya bakteria, fangasi na virusi vya aina mbalimbali. Aidha
husaidia kuzuia magonjwa ya moyo ikiwemo kuondoa lijamu katika mishipa
ya damu na hivyo kusaidia katika kurekebisha shinikizo la damu. Faida
nyingine za vitunguu swaumu ni pamoja na
Kutibu
saratani ikiwemo saratani ya tumbo na utumbo mkubwa. Tafiti zinaonesha
idadi ndogo ya wagonjwa wa saratani katika nchi ambazo wakazi wake wana
utamaduni wa kutumia vitunguu swaumu kwa wingi.
Vitunguu
swaumu husaidia kudhibiti kiwango cha sukari katika damu. Hata hivyo
inashauriwa kwamba wagonjwa wa kisukari wanaotumia sindano za insulin
wasitumie kitunguu swaumu kwa wingi mpaka watakaposhauriwa na daktari.
Huzuia kusanyiko la chembe sahani zinazosaidia kuganda kwa damu (platelet aggregation)
Husaidia ufyozwaji wa thiamin, hivyo kusaidia kuepusha mwili na ugonjwa wa beriberi
Ina kiasi kikubwa cha vitamini C ambayo husaidia kuzuia ugonjwa wa kiseyeye
Hutumika kutibu magonjwa nyemelezi kama toxoplasmosis, hasa kwa watu wenye upungufu wa kinga mwilini.
Ushahidi wa Kitafiti
Katika
utafiti uliofanyika nchini Czech ilionekana kuwa matumizi ya vitunguu
swaumu yalisaidia sana katika kupunguza kusanyiko la lijamu
(cholesterol) pamoja na mafuta yasiyofaa mwilini (low
density
lipoproteins) katika mishipa ya damu. Aidha, mwaka 2007 BBC iliripoti
matumizi ya vitunguu swaumu katika kusaidia kumkinga mtumiaji dhidi ya
aina fulani ya mafua
iliyosababishwa
na virusi. Mwaka 2010, ulifanyika utafiti mwingine ambao ulijumuisha
wagonjwa 50 wenye shinikizo la damu sugu ambalo lilikuwa ni vigumu
kudhibitiwa hata kwa matibabu
yaliyozoeleka
ya dawa na njia nyingine. Kama njia ya kuchunguza ufanisi wa vitunguu
swaumu katika kutibu shinikizo la damu, baadhi ya wagonjwa hao walipewa
vitunguu swaumu wakati
wengine
walipewa dawa isiyohusika na matibabu ya shinikizo la damu (au
placebo). Ilionekana kuwa wale waliopewa vitunguu swaumu kama dawa ya
shinikizo la damu walionesha maendeleo
mazuri
kwa vitunguu swaumu kuweza kushusha vizuri kiwango cha shinikizo la
damu, hususani systolic pressure, tofauti na wale waliopewa placebo.
Nini siri ya kitunguu swaumu?
Sifa
kuu zinazokifanya kitunguu swaumu kuwa na uwezo na faida zilizoainishwa
hapo juu ni kule kuwa kwake na viasili kadhaa (ingredients) ambavyo
vinafanya kazi tofauti tofauti. Uwezo wake wa kiutendaji unatokana na
mambo yafuatayo;
Vina
uwezo wa kusababisha kutanuka kwa mishipa ya damu (vasodilation) kwa
kubadilisha polysulfides zilizopo ndani yake kuwa hydrogen sulfides
kwenye seli nyekundu za damu.
Husaidia
uthibiti wa kiwango cha sukari mwilini kwa kushusha kiwango cha
kemikali ya homocystine na kupunguza madhara ya kisukari.
Iwapo
vitapondwa pondwa vizuri, vitunguu swaumu hutoa kemikali iitwayo
Allicin ambayo ni dawa dhidi ya bateria, na phytoncide ambayo huua
fangasi wa aina mbalimbali.
Harufu mbaya ya kitunguuu swaumu hutokana na gesi aina ya hydrogen sulfide ambayo inayotolewa baada ya kuvila.
Nini Madhara ya vitunguu swaumu?
Ukiacha faida zake, vitunguu swaumu pia vina hasara na madhara mbalimbali kwa mtumiaji. Madhara hayo ni pamoja na;
Harufu
mbaya mdomoni ambayo hutokana na kemikali ya AMS (allyl methyl
sulfide). Harufu mbaya hii, hata hivyo, yaweza kupunguzwa kwa kunywa
maziwa au kunywa maji mengi.
Kwa baadhi ya watumiaji, vinaweza kuwaletea mzio au mcharuko mwili (allergies au inflammatory reactions)
Kichefuchefu, Kutapika na kuharisha.
Huweza
kusababisha hatari ya kuvuja damu, kwa sababu huzuia kazi ya seli
sahani (platelets) zenye kusaidia kuganda kwa damu kushindwa kufanya
kazi yake vizuri, na hususani kwa mama wajawazito, baada ya upasuaji au
mara baada ya kujifungua.
Huingiliana
katika utendaji kazi wake na dawa kadhaa kama vile warfarin,
antiplatelets, saquinavir, dawa za shinikizo la damu kwa ujumla hasa
calcium channel blockers, na antibiotiki za jamii ya quinolone kama vile
ciproflaxacillin.
Aidha, vinaelezwa pia kuwa na madhara kwa wanyama jamii ya paka na mbwa.
FAIDA YA KITUNGUU SAUMU KINATIBU MARADHI MENGI BINADAMU ANAJISAHAU KUTUMIA KITUNGUU SAUMU.
Kitunguu
swaumu hakikosekani katika kila jiko duniani.Ni mmea maarufu sana kwa
tiba.Kitunguu swaumu ni jamii ya yungiyungi.Kitunguu swaumu kilicho bora
zaidi duniani ni kinachotoka misri kwasababu ya tabia ya ardhi yake na
mto nail.Kitunguu swaumu kina harufu ya kipekee isiyowapendeza watu
wengi ingawa kimebeba siri nyingi za tiba.Kwa ajili hiyo maana yake
kilatini ni HARUFU ICHOMAYO.
Ili
kuepukana na harufu ya kitunguu swaumu baada ya kukila,kula tofaa au
tafuna majani mabichi ya naanaa,au kunywa maji yaliyotokosewa
karafuu.Kitunguu swaumu kitapoteza nguvu ya tiba iwapo kitapikwa na kila
kinapowekwa muda mrefu ndipo nguvu zake huongezeka (baada ya majani
yake kukauka kabisa).
Kitunguu
swaumu kimekusanya protin 49%,sulphur 25%,kiasi fulani cha
chumvi,homoni zitoazo nguvu za kiume,viuaji sumu,vikojozavyo,vitoavyo
safura,vinavyoteremsha hedhi,vimeng'enyo vyenye kuyeyusha mafuta na
viini vyenye kuua minyoo.Kila utafiti unapoendelea ndipo faida na
maajabu ya kitunguu swaumu yanapoongezeka.
BAADHI YA MARADHI YANAYOTIBIWA NA KITUNGUU SWAUMU;
1.Kiua sumu
2.Kisafisha tumbo
3.Kiyeyusha mafuta(cholestro)
4.Huzuia mvilio wa damu
5.Kusafisha njia ya mkojo
6.Kutibu amoeba
7.Kuzuia kuhara damu(Dysentery)
8.Tumbo kushindwa kumeng'enya(Indigestion)
9.Gesi
10.Msokoto wa tumbo
11.Typhoid
12.Kidonda kilichooza
13.Dondakoo
14.Mabaka
15.Baridi yabisi(Rheumatisim)
16.Mishipa
17.Uziwi
18.Virusi vya homa ya mafua(Influenza)
19.Mafua
20.Saratani(Cancer)
21.Kifaduro
22.Kifua kikuu cha mapafu
23.Kipindupindu
24.Kutoa minyoo
25.Upele
26.Kuvunjavunja mawe katika figo
27.Mba kichwani
28.Kuupa nguvu ubongo
29.Kuupa nguvu fizi
30.Kuzuia meno kung'ooka
31.Nguvu za kiume
32.Maumivu ya kichwa
33.Kizunguzungu/kisunzi
34.Kutuliza maumivu ya meno
35.Kujenga misuli na kutia nguvu
36.Mkakamo wa ateri(Arteriosclerosis)
37.Shinikizo la damu
38.Kinga ya tauni na ukimwi
39.Magonjwa ya macho
KITUNGUU SAUMU
kimekuwa kikitumika kutibu na kuboresha afya ya mwili na hivyo kumfanya mtumiaji awe mrembo na mwenye afya bora.
Matumizi ya kitunguu saumu kibichi yamekuwa yakisaidia vitu vingi sana mwilini.
Baadhi
ya hayo ni pamoja na kupambana na virusi, bakteria, fangasi na pia sumu
mbalimbali hasa zile zinazosababishwa na baadhi ya vyakula mwilini.
Kutokana na hilo, matumizi ya kitunguu saumu kama tiba na kipodozi, ni jambo linalopendekezwa na wataalamu wa urembo wa asili.
Katika
matumizi yake kitunguu saumu hutumika kwa kula na wakati mwingine
kupaka, ambapo hili hutegemea zaidi na mahitaji au matatizo ya mtumiaji
husika.
Pamoja
na njia hizo nilizotaja hapo juu, lakini wataalamu wanashauri ulaji wa
kitunguu saumu kibichi kila siku, kwani husaidia kuboresha afya ya
muhusika.
Ikiwa
utashindwa kukitafuna chenyewe, unaweza kuchanganya kwenye chakula
kingine ambacho unatumia alimradi tu ukipate kikiwa halisi.
Kwenye urembo, kitunguu saumu husaidia kuondoa matatizo yafuatayo;
Chunusi
Changanya
kitunguu saumu kilichosagwa kijiko kimoja na kijiko kimoja cha juisi ya
ndimu. Chukua pamba na paka sehemu zote zilizoathirika. Kaa na
mchangyiko huo kwa muda wa dakika 15 hadi nusu saa.Ikiwa utaendelea kwa
muda wa wiki moja. Tatizo la chunusi litakuwa limeondoka kabisa.
Kunyonyoka kwa nywele
Ni
kwa muda mrefu sasa kitunguu saumu kimekuwa kikitumika kama tiba ya
kunyonyoka kwa nywele. Unachotakiwa kufanya ni kutumia mafuta yake kwa
kupakaa kwenye ngozi ya kichwa kila siku kabla ya kulala.
Fanya
hivyo mara kwa mara kwa muda usiopungua miezi mitatu na utaona matokeo
yake. Ikiwa utakosa mafuta yake, si vibaya ikiwa utatumia kitunguu
chenyewe kilichosagwa kwa kupaka kwenye ngozi ya kichwa kila siku usiku
na kuosha asubuhi yake.
Fangasi vidoleni
Kupambana
na fangasi kwenye vidole vya miguu na mikono, unashauriwa kutumia
kitunguu saumu kilichosagwa kwa kupaka eneo lililoathirika. Hakikisha
unakaa nacho usiku kucha ukiwa umevaa soksi ama glavu. Fanya hivyo kila
siku hadi utakapoona muwasho na maumivu yameisha.
MBA
Paka
kitunguu saumu kilichosagwa katika ngozi ya kichwa ama sehemu yeyote
iliyoathirika. Hakikisha unatumia hadi pale ugonjwa utakapokuwa
umetoweka kabisa.
MATUMIZI KATIKA NCHIMBALIMBALI:
kitunguu ni kiambatanisho muhimu kidishi kimaendeleo katika sehemu nyingi ulimwenguni.
Zamani Egpta iliheshimiwa kuwa ya hadhi ya kimungu.
MAANDALIZI YA KITUNGUU SAUMU KIMADAWA:
Kitunguu saumu na asali. Jaza chupa ya glasi na vitunguu saumu vilivyomenywa na
kukatwa katwa polepole mwaga katika asali ya kwamba inajaza nyufa katikati ya fundo ya
kitunguu. Weka glasi kwenye sehemu ya joto yenye c 20oc. Katika siku mbili hadi wiki nne,
asali itanyonya juisi ya kitunguu saumu na kitunguu hicho kitachechemea na kutoingiza
mwanga usichuje. Tumia katika muda wa miezi 3.
Kitunguu Saumu dawa ya kikohozi
Ponda kijiko cha chai cha kitunguu saumu katika kipimo hicho hicho cha sukari au asali.
Tumia mara moja k.mf. kwa kikohozi.
Kitunguu saumu mafuta. Weka g 200 za vitunguu vilivyokobolewa saga kitunguu saumu na
kuweka kwenye chombo cha glasi na ongeza mafuta ya kutosha (au vizuri mafuta ya chakula)
funga. Funga jagi kwa kubana vizuri, na weka ikae kwenye sehemu yenye joto kama C 20
kwa siku tatu. Tikisa mara chache kila siku. Halafu weka kwenye sehemu ya baridi, bila
kuchuja. Tumia katika muda wa mwezi mmoja.
Kitunguu saumu „tinkcha“. Loweka g 200 za vitunguu vilivyomenywa na kukatwakatwa
katika lita moja ya brandi au alikoholi 40-50%, kwa siku 14 kwenye C 20° katika chupa
yenye kufungwa vizuri bila kupitisha hewa. Tikisa chupa hiyo mara nyingi kwa siku. Chuja
vipande vya kitunguu saumu. Tinkcha inakaa muda wa mwaka.
MAPENDEKEZO YA MATUMIZI
Kula kitunguu saumu kibichi- hii ni bora.
Tumia katika kupika.
Kula vitunguu saumu vingi kuzuia magonjwa. Kitunguu saumu ni safi sana kwa mfano kuna
usemi kwamba, chakula chako kiwe ndiyo dawa yako, na dawa yako chakula chako. Hii ni
kweli tu, hata hivyo, kwa kitunguu saumu kibichi, kama ilivyo vitu vingi vyenye nguvu
vinaangamizwa katika kupikwa. Vitunguu saumu vibichi vinatia nguvu katika mfumo wa
kinga ya maradhi. Matumizi kawaida ya vitunguu saumu yameonyeshwa katika kupunguza
madhara ya magonjwa ya moyo, kiharusi, kansa, msukumo wa damu na homa ya mafua
Makali (flu).
Tunashauri kwa nguvu ya kuwa wanaoteseka kwa UKIMWI (AIDS) waweke
kitunguu saumu katika chakula chao cha kila siku, kupunguza nguvu ya magonjwa mengine.
Kwa sababu inafanya mara mbili, kwa matumizi ya nje na kwa ndani kama dawa ya kuua
wadudu, vitunguu saumu ni masaada wa kutibu magonjwa yote ya kuambukiza; Toifodi,
minyoo, bilhazia, malaria, damu yenye maambukizo na sumu n.k. Zaidi yake vitunguu saumu
vinaimarisha kumbukumbu, hupunguza shindikizo la damu na Homa, na vinafanya kazi
kupinga ugumu wa kuta za ateri (hardening of arteries). Vitunguu saumu pia vinapinga virusi
na dhidi ya kinyume cha mambo ya fangasi.
1.Majipu au uvimbe na chunjua.
Saga vitunguu saumu vibichi na funga vilivyopondwa kwenye sehemu ya jipu, uvimbe au
Chunjua mara mbili kwa siku na gandamiza. Anza matibabu haya mapema iwezekanavyo.
2. Amiba.
Katakata vitunguu saumu sawasawa vipande vidogo na chukua kijiko kikubwa 1 pamoja na
Chai mara tatu kwa siku (usitafune, kusaidia kupinga kutoa harufu mdomoni). Endelea na
Matibabu haya kwa siku 5. I (H-M Hirt) aliponywa mwenyewe toka Amiba kuharisha
damu kwa Tiba hii.
3. Malaria.
Katakata vitunguu saumu sawasawa. Meza kijiko kimoja cha vitunguu hivi mara tatu kwa
Siku na kunywa lita 2 za limao glasi ya chai kwa siku. Endelea na tiba hii kwa siku 5.
Angalia pia ukurasa wa 8 kwa ajili ya malaria.
4. Kisukari, shindikizo la damu
kinga ya ugumu wa kuta za arteri (hardening of the
arteries).
Kula vitunguu saumu kwa wingi, vitunguu saumu na vitunguu vinapunguza sukari katika
damu na kusawazisha damu ya cholesteroli, na shindikizo la damu. Badala yake chukua
matone 20 ya vitunguu tinkcha mara 3 kwa siku, basi hii ni pungufu ifuatayo:
5. Kikohozi, homa, sinusitis na kuvimba koo.
a) Kula klovu ya vitunguu saumu mara tatu kwa siku.
b) Chukua kijiko cha chai cha kitunguu saumu asali kila masaa machache.
c) Watoto wanaweza kutumia kijiko cha chai cha kitunguu saumu
mchanganyiko kila baada ya masaa machache.
d) Chukua kijiko cha chai cha kitunguu saumu mafuta mara 6 kwa siku.
6. Kandika.
Chukua kijiko cha chai cha kitunguu saumu au kitunguu saumu yenye asali, kila masaa
machache. Weka mdomoni kwa muda mrefu iwezekanavyo.
7. Fangasi inayoambukiza pamoja na ugonjwa wa ukungu kwenye vidole vya miguu.
Funga sehemu zilizoathirika kwa juisi ya vitunguu saumu vibichi vilivyopondwa au
mafuta.
8. Homa ya matumbo na maambukizo mengine.
Kama itatokea homa ya matumbo, bacillary, kuharisha damu, kifua kikuu, kipindupindu,
trypanosomiasis (ugonjwa wa kusinzia): Siku zote ongeza kitunguu saumu kwa tiba ya
kawaida.
9. Kinga ya mishipa ya damu.
Kitunguu saumu siku zote kinafanya damu kuwa laini na kukinga kutengeneza damu
kuganda ambayo inasababisha shida ya thrombosis. Hii ni muhimu kwa wagonjwa wanaolala kitandani kwa muda mrefu.
10. Kuota meno utotoni.
Futa ufizi kwa fundo la kitunguu Saumu.
Kitunguu
thaum kina harufu ya pekee isiyowapendeza watu wengi, ingawa kimebeba
siri nyingi za tiba. Kwa ajili hiyo maanayake kwa kilatini ni : harufu
ichomayo, na kwa kiarabu lugha ya Quraan huitwa: fuum, nayo ndio sahihi
zaidi; kwasababu thaum ni lafdhi ya kihieroglifu ya kifirauni
(hieroglyphic).
Allah S.W amesema:
"
Na (kumbukeni habari hii kadhalika) Mliposea: Ewe Mussa! hatuwezi
kusubiri chakula cha namna moja tu, basi tuombee kwa Mola wako atutolee
vile vinavyooteshwa na ardhi kama mboga zake, matango yake, fuum
(kitunguu thaum) zake, adesi zake na vitunguu vyake." (2:61)
Iliandikwa
katika piramidi (pyramid) huko Misri tangu miaka 4500 iliopita kuwa
kitunguu thaum kilikuwa wakipewa wajenzi ya piramidi. Walikuwa wakila
kitunguu thaum ili wapate nguvu na nishati.
Mwandishi
wa kitabu juu ya tiba zinazotokana na kitunguu thaum alimnasihi mfasiri
wake kuwa " Iwapo unataka nguvu, nishati na uwekevu basi kula tembe ya
kitunguu thaum na glasi ya maji kila siku kabla ya kula chakula. Daud
Al-Antaky ameeleza katika kitabu chake cha Tadhkira kuwa kitunguu thaum
hupoza zaidi ya maradhi 40.
Wale wapiganaji wa miereka wa huko Roma walikuwa wakila kitunguu thaum kabla ya kupigana ili wapate nguvu na wepesi.
Imethibitishwa
kisayansi kuwa kitunguu thaum husafisha damu kutokana na mafuta
(cholestrol) ambayo husababisha magonjwa ya mishipa ya ateri na maradhi
ya moyo, na pia husafisha damu kutokana na vijidudu na maikrobati kuliko
(antibiotic) vengine. Pia imethibitishwa kwa kuzuia kuenea kwa sumu ya
nyoka katika mwili wa mwanaadam na pia husafisha maida kutokana na
vimelea (parasites).
Rais
wa matabibu, Ibn Sina amesema kuhusu kitunguu thaum: "Kitunguu thaum
hulainisha na kuondoa gesi, hutoa vidonda katika ngozi, huhifadhi maji.
Vumbi lake likichanganywa na asli akipakwa mwenye ukoma litamfaa,
kitunguu thaum humfaa mwenye maradhi magonjwa ya mishipa na nyonga
(sciatia). Maji yake (yaliotolewa kwa kupikwa) hutuliza maumivu ya meno,
vilevile hufaa kwa kikohozi.
Kitunguu
thaum kimekusanya protein 49% mafuta muhimu ya sulphur 25% na kiasi
flani cha chumvi, homoni (hormones) zitiazo nguvu za kiume na
vinavyoteremsha hedhi.
BAADHI YA MARADHI YANAYOTIBIWA NA KITUNGUU SAUMU:
Kiua Sumu:
Saga
tembe tano za kitunguu thaum, changanya na asali kikombe kimoja
kilichochanganywa na habbasouda na kunywa papo hapo. Kunywa asubuhi na
jioni. Paka mafuta ya kitunguu thaum pahala panapouma iwapo ni sumu ya
nyoka au paka nje ya tumbo iwapo umekunywa sumu.
Kusafisha tumbo:
Kabla
ya kula chakula, meza tembe za kitunguu thaum na baadae kunywa maji ya
shimari yaliyochanganywa na asali kwa muda wa wiki moja.
Kiyeyusha mafuta (Cholestrol):
Unapokula chakula kila siku, weka katika kachumbari kiasi cha tembe 2 vilivyosagwa ule pamoja na kachumbari.
Kiongeza mkojo chenye kusafisha njia za mkojo:
Chemsha
vizuri hairi, na baada ya kupoa tia tembe 3 za kitunguu thaum
zilizosagwa. Kunywa kinywaji hicho kila siku kabla ya kula na kunywa
juisi ya limau/ndimu.
Kuharisha damu (Dysentery):
Chukua
tembe ya kitunguu thaum uikatekate na uile; fanya hivyo kwa muda wa
wiki moja na bora zaidi ukinywa na mafuta ya zaituni kijiko kimoja.
Gesi na Indegestion:
Kunywa juisi ya pea iliyochanganywa na tembe 3 za kitunguu thaum kabla ya kulala kila siku.
Kutibu Typhoid:
Kata
tembe 5 za kitunguu thaum, changanya ndani ya maziwa ya moto
yaliyochanganywa na asali kunywa kabla ya kulala. Pia paka uti wa mgongo
mafuta ya kitunguu thaum yaliyochanganywa na mafuta ya zeti, na asubuhi
vuta moshi wa kitunguu thaum kwa muda wa dakika 5.
Kidonda kilichooza:
Ponda
kitunguu thaum mpaka iwe laini kama marhamu halafu jifunge nacho kwa
kutumia bendeji, japo kitawasha lakini kitazuia ugonjwa wa gangrene
ambao unaweza ukapelekesha kukatwa kiungo. Vilevile unaweza kusafisha
kidonda kwa kuchanganya kitunguu thaum kilichosagwa kikatiwa maji
vuguvugu (warm water) na kikasafishwa kidonda.
Mishipa:
Kata
tembe za kitunguu kitunguu saumu na umeza kwa maziwa ya moto (sio moto
sana) yenye matone ya ambari kabla ya kulala kila siku, dawa hii huipa
mishipa nguvu.
Homa ya mafua (Influenza):
Kunywa
juisi ya machungwa na juisi ya limau zilizochanganywa na tembe 7 za
kitunguu thaum kunywa juisi hiyo kabla ya kulala. Vuta moshi wa kitnguu
thaum.
Mafua:
Meza
tembe za kitunguu thaum baada ya chakula pamoja na juisi ya kitunguu
thaum iliyochanganywa na juisi ya limau pamoja na kuvuta moshi wa
kitunguu thaum.
Saratani (Cancer):
Katika
kitunguu thaum kuna kiini kinachozuia saratani, kwa kila mgonjwa wa
saratani anashauriwa ale kwa wingi kitunguu thaum na karoti (carrot).
Kifua kikuu (cha mapafu):
Kila asubuhi kabla ya kula chakula meza tembe 3 za kitunguu thaum, saga ule pamoja na mkate na jioni vuta moshi wake.
Kipindupindu (cholera):
Ili
kujikinga na maradhi hayo wakati kikienea, kula kijiko kimoja cha
kitunguu thaum kilichosagwa na kukorogewa katika asali baada ya kila
chakula.
Kutoa minyoo:
Ponda
tembe 3 za kitunguu thaum, tia ndnai ya maziwa na kunywa (bila kutia
sukari) jioni kabla ya kulala na asubuhi kunywa mafuta ya mbono.
Upele:
Chukua
tembe 5 za vitunguu thaum uvisage na uvikoroge katika shahamu na paka
pale penye upele kuazia jioni mpaka asubuhi na ukoshe kwa maji ya moto
tumia kwa muda wa wiki moja.
Mbaa kichwani:
Ponda
uzuri vitunguu thaum 3 na uvikoroge katika siki ya tofaha (Apple
vinegar) katika chupa ya bilauri (sio plastiki) na uache juani kwa muda
wa wili moja. Baada ya hapo jipake kichwani pamoja na kusugua kwa muda
wa wili 1 na baada ya wiki jipake mafuta ya zeituni.
Nguvu za kiume:
Saga
kitunguu thaum kitie ndani ya mafuta ya zeti na weka katika moto mdogo
mdogo mpaka iwe rangi ya manjano na tia katika chupa na wakati wa haja
jipake katika dhakari na osha baada ya saa moja.
Kujenga misuli na kutia nguvu:
Kila
siku kabla ya kula kunywa kikombe kikubwa cha maziwa ya ngamia
yaliyotiwa tembe 2 za kitunguu thaum iliyosagwa. Kunywa kwa muda wa
mwezi mmoja mfululizo.
Kinga ya taunni na ukimwi:
Ngao
kubwa ya maradhi mabaya ni Kumcha Allah S.W mwanzo na mwisho wa siku.
Chukua juisi ya kitunguu thaum uichanganye na asali na unywe utafanya
hivo pamoja.
KITUNGUU SAUMU.
tangu
kale kimekuwa kikijulikana kama 'dawa ya kushangaza' na kutumiwa na
watu wengi katika kutibu mafua na influenza. Miongoni mwa faida za
kitunguu swaumu ni kuzuia kupatwa na magonjwa mbalimbali na maambukizo
ya virusi. Hivyo kitunguu swaumu hujulikana kama antibiotiki ya asilia.
Uchunguzi umeonyesha kwamba kula kitunguu swaumu kunapunguza kushadidi
ugonjwa wa influenza na hata kuzuia kupatwa na ugonjwa huo. Vilevile
kula kila mara kitunguu swaumu, huzuia kupatwa na magonjwa ya moyo,
kwani kitunguu swaumu huzuia damu isigande kwenye mishipa ya damu.
Halikadhalika
kitunguu swaumu ambacho pia ni kiungo muhimu cha chakula kina
potassium, na hivyo watu wenye ugonjwa wa shinikizo la damu wanashauriwa
kula vyakula vilivyopikwa kwa kitunguu swaumu.
Si
vibaya kujua kuwa katika uchunguzi uliochapishwa mwaka 2001, imeelezwa
kwamba, kitunguu swaumu kina athari kubwa na nzuri pale kinapochanganywa
na baadhi ya dawa nyinginezo katika kutibu Ukimwi au HIV.
Haya shime jamani… kuanzia leo vyakula visikose kuungwa na kitunguu thomu, iwapo unaogopa kupatwa na influenza kama mimi!
MADHARA YAKE:
Kitunguu saumu kinaweza kukera ngozi hasa baada ya kutumia kwa muda mrefu. Epuka
kuhusisha kwenye macho.
Post a Comment