Inafurahisha kuona kuwa wapo
wafanyabiashara wengi maeneo tofauti tofauti Nchini mwetu na mitaa tofauti
tofauti wanaouza juisi ya miwa.
Kimsingi juisi hii ni sukari halisia
ambayo haijachakatwa.
Sukari halisia ni nzuri kwa mwili kwani ina virutubisho
na madini kwa wingi.
Miwa ina faida nyingi kiafya. Juisi
ya miwa inafahamika na wataalamu wa afya kwa kuwa na uwezo wa kuupa mwili nguvu
kwa sababu ya ‘glucose’ iliyopo.
Kijiko kimoja cha juisi ya miwa,
kina kalori 11. Madini halisi na vitamin zinazopatikana katika sukari ni kama
phosphorus, calcium, madini ya chuma na potassium.
Si hivyo tu, miwa ni jamii ya tunda
lenye alkali hivyo lina uwezo wa kupambana na saratani hasa ile ya kibofu cha
mkojo na saratani ya maziwa.
Miwa ina upekee wake kwani ina uwezo
wa kuongeza maji mwilini, inaupooza mwili na kuupa nguvu.
Virutubisho vilivyopo katika miwa
vina manufaa makubwa katika kusaidia utendaji kazi wa ogani muhimu kama figo,
moyo, ubongo na viungo vya uzazi.
Pia, wagonjwa wa kisukari wasihofie
sukari iliyopo kwenye miwa kwani haina madhara yoyote kwao. Uzuri wa juisi ya
miwa ni kuwa sukari yake ni halisia.
Post a Comment