
Jeshi
la Polisi limekita kambi Temeke mikoroshini kata ya Sandali jimbo la
Temeke baada ya hali kuelezwa kuonekana tofauti kutokana na vijana wa
eneo hilo kujaa kwa wingi kwa kile kinachoelezwa wanataka matokeo
yatangazwe kwani wana wasi wasi na utangazwaji wa matokeo.
Wananchi hao wanadai kuwa wana wasiwasi kutangazwa matokeo tofauti
wakati wanaamini mgombea wao kutoka CUF atakuwa kashinda dhidi ya
CCM,lakini bado mawakala hawajaweka wazi matokeo hivyo hadi sasa.
Kwa Mujibu wa muandishi wetu Sam Mahela aliyepo eneo hilo anayefuatilia
taarifa hizi za uchaguzi anasema kuwa licha ya jeshi la polisi kuwepo
eneo hilo linahakikisha hakuna tatizo lolote linalo tokea na kuona
wasimamiziwakitangaza matokeo bila hofu
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.