Wagombea urais wa vyama vya CCM na Chadema wanachuana vikali kwa mujibu wa matokeo ya awali yaliyotangazwa kwenye vituo mbalimbali nchini baada ya wananchi kupiga kura jana.

Matokeo hayo ya awali yanaonyesha kuwa Dk John Magufuli wa CCM na Edward Lowassa wa Chadema wanapishana kwa kura chache kwenye vituo ambavyo kura zimeshahesabiwa, huku kukiwa na tofauti kubwa kwenye kura za ubunge.

Katika Jimbo la Musoma Mjini, Beldina Nyakeke anaripoti kuwa matokeo ya urais kituo cha CGS Shule ya Msingi Musoma B, Dk John Magufuli, CCM amepata kura 169, Edward Lowassa wa Chadema (124), Anna Mgwira, ACT-Wazalendo (1), Chief Yemba, ADC (1), Janken Kasambala, NRA (0), Fahmi Dovutwa, UPDP (0), Macmillan Lyimo, TLP (0) na Hashim Rungwe, Chaumma (0).

Kura zilizopigwa 297 zilizoharibika 2

Kwa upande wa kura za ubunge katika kituo hicho Vedastus Mathayo wa CCM (173), Vincent Nyerere, Chadema (119), Eliud Esseko, ACT Wazalendo (1), Gabriel Ocharo, CUF (1), Chrisant Nyakitita (DP) 0, Maimuna Matola (ADC) 0, Ibrahimu Selemani, Tadea (0), Rutaga Sospeter, AFP (0) na Makongoro Jumanne, UMD (0). Kura zilizopigwa ni 297 na zilizoharibika 3.

Katika kituo cha Kitaji, Ofisi ya Kata Jimbo la Musoma Mjini matokeo ya ubunge, Vedastus Mathayo (CCM ), 167, Vincent Nyerere, Chadema (102), Eliud Esseko, ACT Wazalendo (1), Gabriel Ocharo, CUF (0), Chrisant Nyakitita, DP (0), Maimuna Matola, ADC (0), Ibrahimu Selemani, Tadea (0), Rutaga Sospeter, AFP (1) na Makongoro Jumanne, UMD (0).

Kwa upande wa matokeo ya urais, katika kituo cha Kitaji ofisi ya Kata, Dk Magufuli (167), Lowassa (104), Mgwira (1), ADC, NRA, UPDP, TLP na Chaumma hazijapata kura.

Katika kituo cha John Bosco, Dk Magufuli (143), Lowassa (82), Mgwira (3), Yemba (1) na Rungwe (1).

Kwa upande wa ubunge, Mathayo (145), Nyerere (79), Eliud Esseko (2), na Gabriel Ocharo (1).

Katika Jimbo la Monduli Peter Saramba anaripoti kuwa matokeo ya ubunge katika kituo cha NMC B, Namelok Sokoine wa CCM (58), Julius Kalanga wa Chadema (137), Navaya Ndaskoi, ACT-Wazalendo (1).

Katika kituo hicho matokeo ya urais Mghwira wa ACT-Wazalendo (2), Lowassa (Chadema) 150, Dk Magufuli (CCM) 39, Rungwe (Chaumma) 01.

Kwenye kituo cha NMC A matokeo ya ubunge ni Namelok Sokoine (CCM) 38, Julius Kalanga (Chadema) 169, Navaya Ndaskoi (ACT-Wazalendo) 01.

Kwa upande wa urais kituo cha NMC A, Mghwira (ACT-Wazalendo) 0, Lowassa 178, Dk Magufuli (CCM) 30, Lyimo 0.

Kutoka Dodoma Mjini, Sharon Sauwa anaripoti kuwa katika matokeo ya urais kituo cha Mwangaza-1, Mghwira (2), Dk Magufuli (156) na Lowassa (131).

Kwa upande wa ubunge kituo hicho, Christina Alex wa ACT Wazalendo (5), Antony Mavunde, CCM (144) na Kigaila Singo, Chadema (135).

Salma Said anaripoti kutoka Pemba kuwa katika Kituo cha Skuli ya Bwagamoyo, Jimbo la Mtambwe wilayani Wete, Pemba katika Kituo Namba 1, Maalim Seif Sharrif Hamad amepata kura 317 na Dk Mohamed Shein 5, wakati kituo Namba 2- Maalim Seif (220), Dk Shein (2).

Katika kituo cha Gombani Station (1),(2) na (3) jimbo la Wawi, Mkoa wa Kusini Pemba, Kelvin Matandiko anaripoti kuwa kituo cha Station 1, Dk Shein (18), Maalim Seif (258), Hamad Rashid (4). Jumla ya kura 282 na zilizoharibika 2.

Katika kituo cha Station 2, Dk Shein (21), Maalim Seif (246), TLP (1), ADC (1), ACT (1), Tadea (1) na SAU(1). Jumla ya kura ni 275 na zilizoharibika ni 3. Matokeo hayo yalitolewa na msimamizi mkuu wa kituo cha Gombani Stadium, Abubakar Shaame Faki.

Katika Jimbo la Shinyanga Mjini, Suzy Butondo anaripoti kuwa mtokeo ya awali ya urais katika kituo cha Uwanja wa Soko Mageuzi kuwa Dk Magufuli (134), Lowassa (104), Mghwira (1) na wagombea wengine hawakupata kura.

Kwa upande wa ubunge katika kituo hicho, Steven Masele wa CCM (112), Patrobas Katambi, Chadema (127), Nyangaki Shilungushela wa ACT Wazalendo (1).

Katika jimbo la Moshi Mjini kituo cha Shule ya Msingi Mawenzi- 1, Mngwira (1), Dk Magufuli (89), Lowassa (131) na Lyimo (1).

Kwa upande wa ubunge katika kituo hicho Jafary Michael, Chadema (150), Davis Mosha, CCM (83) na Marchel Kitali, (UDP (1).

Katika kituo cha Shule ya Msingi Mawenzi-2, Lowassa (143), Dk Magufuli (94) na Rungwe (1).

Kwa upande wa ubunge katika kituo hicho, Buni Ramolewa ACT Wazalendo (1), Mosha, CCM (78), Michael, Chadema (139).

Katika jimbo la Nyamagana, Midraji Ibrahim anaripoti kuwa matokeo ya ubunge kituo cha Calfonia Majengo Mapya B, Chaha Okong’ wa ACT Wazalendo (1), Mabula Stanslaus, CCM (152), Wenje Ezekia, Chadema (99), Faida Hassan, CUF (1), Mohamed Juma, Jahazi Asilia (0), Ahmed Mohamed, NRA (2) na Ramadha Uhadi wa UDP hakupata kitu.

Kwa upande wa urais Mgwira (0), Dk Magufuli (170), Lowassa (85) na waliosalia wamepata 0.

Hawa Mathias anaripoti kutoka Mbeya Mjini kuwa katika kituo cha Mwasyoge kura za urais Dk Magufuli (85), Lowassa (128).

Kwa upande wa ubunge Joseph Mbilinyi wa Chadema (147) na Shambwee Shitambala wa CCM (63).

Katika kituo cha Kajigili, kura za urais Dk Magufuli (105) na Lowassa (96).

Kwa upande wa ubunge Joseph Mbilinyi (105), na Shambwee Shitambala (95).

Katika kituo cha Mifugo B, Lowassa (104) Magufuli (139), na Mghwira (7).

Kutoka Pemba, Salma Said anaripoti kuwa matokeo ya awali katika Kituo cha Skuli ya Bwagamoyo Wilaya ya Wete, Pemba , Kituo namba moja, Jimbo la Mtambwe, Maalim Seif amepata 317 na Dk Mohamed Shein (5).

Kituo Namba 2, Maalim Seif (220) na Dk Shein (2).

Post a Comment

POPULAR POST

 
Top