1. Siku ya Valentines Day asili yake ni kutoka Dola ya Warumi. Ni siku ya kumbukumbu (memoria day) na sehemu nyingine ni (festum) maana yake siku kuu ya daraja la kwanza kwa kumkumbuka Padre Valentine aliyeuawa na utawala wa kirumi

    Sababu ya kutetea waumini wake kufunga ndoa badala ya kuishi na vimada tu. Lakini sikukuu hiyo imeenea sana katika nchi za magharibi na baadaye karibu sehemu kubwa ya ulimwengu kuisherehekea kama siku yamapenzi kinyume cha dhamira ya Mt. Valentine.

    Watawala wa dola ya kirumi walikuwa na fikra za kueneza dola ya kirumi duniani kote na hivyo vijana hawakutakiwa kuoa, ili wawe huru muda wote kwenda vitani kupigania nchi.

    Wakioa hawangekuwa na uhuru wa kwenda vitani bali kuwa na famiia zao. Vijana wengi wakawa na mtindo wa kuwa na vimada tu kitu ambacho kanisa lilikukwa linapinga.

    Padre Valentine ambaye alikuwa Roma akawa anawahimiza vijana kufunga ndoa badala ya kufanya ngono bila ndoa kwani ni dhambi na kitu kisichokubalika mbele ya Mungu.

    Akawa anafungisha ndoa kwa siri kwenye makatakombe (mahandaki chini ya kanisa ambako kuna sehemu za ibada kwa watu wachache), alifanya hivyo kwa vile kufunga ndoa hadharani ilikuwa ni kukiuka amri ya wakuu wa dola ya kirumi.

    Baadhi ya watu walifichua siri hiyo, hivyo Padre Valentin alishikwa na dola ya Warumi na kuuawa kama shahidi mfia dini kwa ajili ya kutetea waamini wake wafunge ndoa badala ya maisha ya ngono zembe bila ndoa.

    Wakristo wakawa siku ya kumkumbuka Padre Valentin kama mfia dini sababu ya kutetea maisha ya wanakanisa kuwa wanandoa. Ikaenea katika kanisa nchi za magharibi na hata duniani ambako wanakanisa wanamkumbuka Mt. Padre Valentin.

    Baadaye ikapokeleka na watu hata wasio na imani ya kikristo kama ni siku ya kufanya kumbukumbu kwa Mt. Valentin kama mtetezi wa Ndoa.

    Maudhui ya siku hiyo kwa wasiowanakanisa imechukua maana nyingine ya kwamba ni siku ya wapendanao hata kwa wasio wanandoa bali mradi wanapendana, kitu ambacho ni kinyume cha malengo ya mfia dini Mt. Padre Valentin aliyetaka vijana wafunge ndoa badala ya kuwa na hawara tu (vimada).

     

  2. Mtakatifu Padre Valentino alifanya jitihada kuwaepusha vijana na dhambi ya uasherati na kuwahimiza kuchagua wa kuwa nao kimaisha kwa kufunga ndoa. Ndicho alichokazania kuwahimiza vijana waliokuwa wanajeshi wafunge ndoa wakati serikali haikutaka vijana wafunge ndoa wasiwe wanatoroka kwenda kwa wake zao.

    Leo tunasherehekea sikukuu yake na walimwengu wamegeuza ni siku ya wapendanao hata wasiowanandoa au wanandoa watarajiwa, ni kwenda kinyume kabisa cha malengo ya asili na teologia ya maana halisi aliyofanyia kazi utume Mt. Valentino.

     
  3.  
    Siku ya valentine ni kila mwezi wa pili ambapo watu hudhihirisha mvuto na haiba za mapenzi kwa kila mmoja kwa kupeana kadi na zawadi.

    Sherehe hii chanzo chake ni mambo ya dini za kirumi.

    Lupercalia ni sherehe iliyoadhimishwa na Warumi wa zamani kila mwezi wa pili tarehe kumi na tano. Lengo lake ilikuwa kuwaheshimu miungu Lupercus na Faunus na ndugu mapacha wawili ambao ni Romulus na Remus ambao huaminiwa kuwa waanzilishi wa mji wa Rumi.

    Sherehe za Lupercalia zilifanyika juu ya kilima kiitwacho Palatine ambapo warumi wa zamani walijenga nyumba zao.

    Makuhani wa miungu lupercus walivaa mavazi ya ngozi ya mbumzi. Baada ya kutoa kafara ya mbuzi na mbwa, walijipaka damu ya mbuzi na mbwa kwenye miili yao, walikimbia kuzunguka kilima wakiwa wamebeba usinga wa ngozi ya mbuzi ulioitwa Februa(kifaa cha utakaso).

    Wanawake wa Kirumi walisimama kando ya Kilima cha Palatine ili wale makuhani waweze kuwapiga na ule usinga/ februa wakiamini kwamba tendo hilo litawasaidia kuwa na uzao mwingi na wepesi wakati wa kujifungua.

    Pia sherehe hii ilihusiana na vijana wa kiume na wa kike kuchagua mpenzi. Makuhani waliweka majina ya wasichana kwenye boksi na kila mvulana alichukua karatasi ya jina la msichana kwenye boksi na msichana huyo atakuwa mchumba wake mpaka sikukuu nyingine ya Lupercalia.

    Mwaka 270 A.D, Sikukuu ya Lupercalia iligeuzwa na kuwa sikuu inayoitwa ya kikristo Kumuheshimu mtakatifu Valentini aliyeuwawa karne ya tatu

    Kuna hadidhi nyingi kuhusu Valentini.
    Kuna hadidhi inayosema valentini alikuwa mkristu aliyekuwa rafiki ya watoto wengi, warumi wakamfunga kwa sababu ya kukataa kutambikia miungu yao. Watoto wakapeleka kadi zenye maneno ya upendo na kuppachika kwenye Vizingiti vya dirisha la chumba cha gereza alimokuwamo Valentini.

    Hadithi nyingine inasema Valentini alimponya binti wa mfungwa mwenzake na baadae huyo binti kuangukia kwenye penzi la Valentini.

    Inaaminiwa kuwa valentini aliuwawa Februari 14 mwaka 269 A.D.
    Mwaka 496A.D Papa aliamuru Februari 14 kuwa sikukuu ya valentini. Ikawa ianasheherekewa na kanisa kama mbadala wa sikukuu za kipagani.

    Chanzo: Kitabu cha GLOBAL HISTORY AND GEOGRAPHY, the grouth of ccivilizations kilichoandikwa na HENRY BRUN, LILLIAN FORMAN na HERBERT BRODSKY


Post a Comment

POPULAR POST

 
Top