John Woka ni msanii ambaye Tanzania ilikuwa nae sana kwenye chati za muziki wa bongofleva kupitia kundi la Watukutu, na sasa Tanzania imepata taarifa za kifo chake kilichotokea alfajiri ya February 16 ikiwa ni saa kadhaa tu baada ya kupelekwa Hospitali.
Woka amefariki baada ya kupata ajali  wakati anatengeneza gari Sinza kwenye mfumo wa AC inasemekana kuna kitu kilifyetuka baada ya kufungua AC na kumpiga kwenye paji la uso na kuingia kama inchi 3 au 2 hivyo damu nyingi zikaanza kumtoka kichwani na mpaka anafikishwa hospitali, Woka alikuwa katika chumba cha wagonjwa Mahututi.
Kifo cha John Woka ni pengo jingine kwenye bongofleva, alipita kwenye chati mbalimbali za muziki huu kutokana na nyimbo zake kama mganga na hii kitu hii ambazo alizipiga kwa kurap kama mlevi.

16 Feb 2016

Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

POPULAR POST

 
Top